KADINDA AMUANIKA MPENZI WAKE
MWANAMITINDO maarufu
Bongo, Martin Kadinda ameamua kumuweka wazi mpenzi wake ambaye siku za
nyuma alikuwa na mpango wa kufunga naye ndoa mapema mwaka huu lakini
kukatokea tofauti kidogo
wakahairisha zoezi hilo.
Mwanamitindi maarufu Bongo, Martin Kadinda akiwa na mpenzi wake.
Akizunguza na mwandishi wa habari hivi karibuni, Kadinda aliweka wazi
kuwa huyo ndio mke wake mtarajiwa na Mungu akipenda watafunga naye ndoa
mwakani. “ Ni kweli ni mpenzi wangu nampenda sana na Mungu akipenda
ndiye mke wangu ambaye nitafunga naye ndoa mapema tu mwakani na Mungu
atusimamie katika hilo,” alisema Kadinda.
0 comments: