Shule yampiga marufuku mwanafunzi kuhudhuria masomo kwa hofu ya Ebola.
Baba wa mtoto huyo ameitaka mahakama kutoa amri kwa shule iliyopo
Milford, Connecticut Marekani kumruhusu mtoto wake aendelee na masomo
kwa kuwa hakuonesha dalili zozote za kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo.
Shule hiyo haikutoa jibu lolote kuhusiana na maombi ya mzazi huyo, kitu
kilichompelekea kufungua mashtaka katika mahakama ya wilaya ya
Connecticut.
Mtoto huyo amekumbana na kadhia hiyo baada ya kusafiri kwenda na kurudi
Lagos, Nigeria akiwa na baba yake kati ya tarehe 2 na 13 Oktoba, ndipo
shule hiyo ilimzuia mwanafunzi huyo kuhudhuri masomo shuleni mpaka
tarehe 3 mwezi Novemba na badala yake shule itakuwa ikimtumia mwalimu
kwa ajili ya kumfundisha akiwa nyumbani kwao.
Tangu kulipuka kwa Ebola katika nchi za Afrika Magharibi, kumekuwa na
mfululizo wa matukio ya kutengwa kwa watu wanaotokea Afrika Magharibi
nchini Marekani ambapo chuo kimoja Texas kilisitisha kupokea maombi ya
kujiunga na masomo kwa watu kutoka Nigeria kwa hofu ya maambukizi ya
virusi vya ugonjwa huo.
0 comments: