KAMANDA WA KUKAMATA MADAWA WA KULEVYA NZOWA ATUMIWA PAKA 3 OFISINI
MAAJABU! Paka
watatu wenye macho mekundu walimshangaza Kamanda wa Polisi Kikosi cha
Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, SACP Godfrey Nzowa
pale alipowakuta katika mlango wa ofisi yake na kumng’ang’ania miguuni.
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, SACP Godfrey Nzowa akiwa ofisini kwake.
Sakata hilo lilitokea wiki iliyopita
wakati Kamanda Nzowa akitoka ofisini na mgeni wake aliwakuta paka hao
mlangoni.Kufuatia hali hiyo, wageni na baadhi ya askari anaofanya nao
kazi walionekana kushangazwa na tukio hilo huku wakijiuliza kwa nini
paka hao wamzingire kamanda huyo na kuwaacha watu wengine?
Hata hivyo, baadhi ya wageni waliokwepo
walihisi kuwa huenda paka hao walitumwa kishirikina na watu anaopambana
nao kwa kuwakamata kutokana na kupatikana na madawa ya kulevya kwani
ameweza kwa kiasi kikubwa kudhibiti biashara hiyo haramu hapa nchini.
Akizungumza na Uwazi, askari mmoja
alisema Kamanda Nzowa amekuwa akipata vitisho na majaribu ya kila aina
ikiwemo rushwa lakini kwa kuwa ni mcha Mungu mzuri anashinda.
Hadi wageni hao wanaondoka paka hao bado walikuwa wamemng’ang’ania kamanda huyo.
Hata hivyo, kamanda huyo alirudi nyuma na kufunga mlango na kuwaacha paka hao wakiwa wamesimama nje ya mlango wa ofisi yake.
Hata hivyo, kamanda huyo alirudi nyuma na kufunga mlango na kuwaacha paka hao wakiwa wamesimama nje ya mlango wa ofisi yake.
Mwandishi wetu alipomuuliza Nzowa
kutokana na hali hiyo alisema ni mambo ya kawaida kwake na
kinachomsaidia ni Mungu kwani kila mara amekuwa akisali.
0 comments: