Nzowa asema dawa za kulevya alizokamatwa nazo Chid Benz ni Heroine

 
Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa amesema dawa za kulevya alizokamatwa nazo rapper Rashidi Abdallah Makwiro a.k.a Chidi Benz katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Ijumaa iliyopita (Oct. 24) ni aina ya Heroine.
Alikuwa na dawa Heroine kete 14″, amethibitisha Nzowa kupitia 255 ya XXL ya Clouds Fm. “na tunaendelea kumhoji tuone kama alipewa au nini kwasababu katika kupatikana iwe umepewa kwa hifadhi au kwa nini bado hiyo ya kupatikana inakutosha, kwasababu hakuna mtu anayepaswa kupatikana na dawa za kulevya. sisi whether unatafutwa siku nyingi hutafutwi siku nyingi kwa wakati huo huo tunapokukuta na hizo unakuwa in for it, na ndio maana sheria inasema hakuna hata defense…sisi tunashukuru kutokana kwamba amekamatwa kwasababu ni dawa hizo za kulevya imethibitika ni dawa za kulevya inatosha.”

Kamanda Nzowa ameongeza kuwa kwa sasa wanaendelea kumhoji na utaratibu utakapokamilika atapandishwa mahakamani.

0 comments: