KIGWEMA, BEST NASSO: TUTAKUKUMBUKA SIDE BOYXX
Wasanii
Best Nasso kushoto, Hamisi Kibiti ambaye ni Meneja wa Best Nasso na
kulia ni msanii Kigwema kwenye picha ya pamoja wakiwa safarini kuelekea
Lindi kwenye mazishi ya msanii mwenzao.
Mdogo
wa msanii Side akiwa kwenye picha ya pamoja na Best Nasso, Kigwema na
waombolezaji wengine mara baada ya kufika mkoani Lindi.
Wasanii wa muziki wa Bongo Fleva, Best
Nasso na Kigwema wamefunguka kuwa daima watamkumbuka msanii mwenzao,
Side Boy aliyefariki mapema jana kwa upungufu wa damu katika Hospitali
ya mkoa wa Lindi.
Wakizungumza na mwandishi wetu kwa njia
ya simu wakiwa njiani kuelekea msibani mkoani Lindi, wasanii hao
walisema kuwa watamkumbuka marehemu siku zote kwa kuwa walikuwa marafiki
wakubwa ndani na nje ya muziki na kuongeza kuwa ni msanii pekee
aliyekuwa akiimba nyimbo zenye meseji zenye kugusa maisha ya watu kwa
kujali zaidi ujumbe na siyo soko kama wanamuziki wengine.
“Hakuna neno tutakaloweza kusema
kuelezea hisia zetu. daima tutamkumbuka Side Boy kama msanii mwenzetu,
rafiki na kaka yetu. RIP”
0 comments: