Historia
kubwa imewekwa muda huu hapa viwanja vya jangwani jijini dar es salaam
Tanzania Ambapo vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi ukawa muda
huu wamesain mkataba ambao unawafanya wao sasa kuungana na kuzungumza
lugha moja ya kuhakikisha kuwa wanafika mbali zaidi wakiwa pamoja,umoja
huo ambao unaundwa na CHADEMA,CUF,NCCR MAGEUZ pamoja na NLD muda huu
wamesaini kwa pamoja makubaliano hayo mbele ya wanachama wao maelfu
waliojitokeza katika viwanja hivyo hapa jijini dar es salaam.
Akizungumza na wanachi waliojitokeza
hapa katibu mkuu wa chadema aesema kuwa makubaliano hayo sio makubaliano
ya vyama na viongozi wakuu bali ni makubaliano ya wanachi wote ambao
wanapenda haki na amani ya tanzania.
mtu wangu hapa kuna picha za shuguli
hiyo ya kusaini makubaliano hayo na tutazidi kukupa kile kinachojiri
hapa uwanja wa jangwani.
|
Wenyaviti
wa vyama hivyo kwa pamoja wakisaini makubaliano hayo ambayo yanawaweka
pamoja na kufanya siasa ya Tanzania kuingia katika historia nyingine
kubwa na ambayo haijawahi kutokea |
|
Mamia ya wanachama waliojitokeza hapa |
|
Naibu katibu mkuu zanzibar chaderma salum mwalim akizungumza lugha ya tatu. |
|
Maalim seif yupo hapa |
0 comments: