ROSE NDAUKA HAKAMATIKI
Acha kabisa! Baada
ya kuachana na aliyekuwa mchumba’ke, Malick Bandawe kisha kurudi kwao,
Kigogo jijini Dar, staa grade one wa Bongo Movies, Rose Donatus Ndauka
anadaiwa hivi sasa hakamatiki hivyo hakauki viwanja.
Uchunguzi wa Ijumaa Wikienda ambalo limekuwa likimnyatia kwa ukaribu
Rose unaonesha kwamba tangu ametengana na mwanaume huyo amekuwa huru
kupita maelezo huku akionesha jeuri ya fedha kama ilivyokuwa kwa mastaa
wenzake, Wema Isaac Sepetu na Kajala Masanja.
Pia uchunguzi huo ulibaini kwamba, mara tu baada ya kutoka ‘kifungoni’,
Rose aliangusha bonge la sherehe ya ‘bethidei’ yake ndani ya Ukumbi wa
Hoteli ya Collosseum, iliyopo Kariakoo jijini Dar na ndiko alikoanza
kuonesha jeuri ya fedha.
Data zilionesha kwamba siku tishio ni ile ya Oktoba 18, mwaka huu ambapo
Rose alikuwa kinara wa ushangiliaji wa timu yake ya Yanga, jambo ambalo
siku za nyuma alikuwa hafanyi hivyo.
Siku hiyohiyo, baada ya kutoka uwanjani alikwenda kubadilisha mavazi yake ya njano na kijani kisha akatupia pamba za kuruka viwanja, akaibuka katika Tamasha la Fiesta kwenye Viwanja vya Leader, Kinondoni jijini Dar.
Siku hiyohiyo, baada ya kutoka uwanjani alikwenda kubadilisha mavazi yake ya njano na kijani kisha akatupia pamba za kuruka viwanja, akaibuka katika Tamasha la Fiesta kwenye Viwanja vya Leader, Kinondoni jijini Dar.
Akiwa ndani ya Leaders, Rose aliambatana na Mtangazaji wa Times FM,
Khadija Shaibu ‘Dida’ ambapo alikuwa akihaha kumnasa mwanamuziki wa
Marekani, T.I aliyetimba Bongo kutumbuiza kwenye tamasha hilo.
Kama hiyo haitoshi, Alhamisi iliyopita, Rose alithibitisha kwamba kwa
sasa hashikiki kwani alitimba kwenye pati ya bethidei ya shoga’ke, Dida
iliyofanyika nyumbani kwake, Mwananyamala, Dar ambapo alikuwa kinara wa
kujiachia kwa kusakata muziki na kumwaga ‘madolari’.
Ulipofika muda wa muziki, hapo ndipo Rose alipopagawa na kujikuta akikata mauno huku akipiga kelele ‘raha jipe mwenyeweee…’
Mwanahabari wetu alipotaka kujua kulikoni Rose kujiachia kiasi hicho, aliomba aachwe afurahie maisha.
0 comments: