MAUAJI YA KUTISHA LUDEWA NJOMBE, ATANDIKWA NONDO KICHWANI HADI AKAFA
Jeshi la polisi wilayani Ludewa likiondoka eneo la tukio
majirani wakiuangaliwa mwili wa marehemu Mgimba.
Mtu
mmoja aliyefahamika kwa jina la Merkion Mgimba(Msuruisi) miaka 70
mkazi wa Ludewa Kijijini katika wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe ameuawa
kwa kupigwa nondo kichwani usiku wa kuamkia tarehe 28 oktoba 2014 akiwa
nyumbani kwake na watu wasiojulikana.
Akitoa
taarifa katika eneo la tukio mke wa marehemu Bi.Theodora Luoga alisema
kuwa marehemu alitoka ndani majira ya saa 5 usiku kwa lengo la
kujisaidia haja ndogo lakini ghafla alikutana na mtu nje ya nyumba yake
na kuanza kupambana naye ndipo alipozidiwa nguvu na kukimbilia ndani
akipiga kelele.
Bi.Theodora
alisema baada ya kusikia kelele hizo sebuleni alilazimika kutoka
chumbani ili aende kutoa msaada kwa mume wake lakini alipofungua mlango
wachumbani alikutana na nondo iliyompata mkononi ndipo alipofanya uamuzi
wa kutokea dirishani ili aende kuomba msaada lakini juhudi hizo
hazikuzaa matunda kwani alishuhudia mtu aliyevalia shati jeupe
akitokomea gizani.
Alisema
baada ya muuaji huyo kukimbia alirudi kuona hali ya mumewe lakini
alimkuta tayari ameshaaga Dunia,hapo akachukua uamuzi wa kwenda
kuwaeleza majirani na kiongozi wa mtaa ili kumsaka muuaji huyo ambaye
hakuweza kumfahamu zaidi ya kushuhudia shati lake jeupe.
“Nilisikia
mumewangu akikimbia kutoka nje na baadae kelele sebuleni ndipo
nilipotoka ili kutoa msaada lakini nilipofungua mlango wa chumbani
muuaji huyo alinipiga na nondo mkononi ikanilazimu kufunga mlango na
kurudi chumbani nikisikia mume wangu akilia kwa uchungu,nikaamua kupitia
dirishani ili niombe msaada kwa majirani ndipo nilipomuona muuaji huyo
akikimbia kichakani”,Alisema Bi.Theodora.
Alisema
muuaji huyo hajachukua kitu chochote zaidi ya kufanya mauaji,pia
alithibitisha kuwa hii ilikuwa ni awamu ya pili kwani kunakipindi
marehemu aliwahi kupambana na mtu nje ya nyumba yake nyakati za usiku na
kumshinda mtu huyo alibeba nondo kama ilivyokuwa leo ila hakutambulia.
Aidha
kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Njombe SACP Fulgence Ngonyani
amethibitisha kutokea tukio hilo alisema mpaka sasa bado jeshi la polisi
linaendelea na upelelezi wake ili kumbaini muujia taarifa kamili
zitatolewa upelelezi ukikamilika.
0 comments: