MHE. BERNARD MEMBE AKABIDHI HUNDI YA $ 100,000 KWA MTOTO WA BRIGEDIA JEN. MSTAAFU HASHIM MBITA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K.
Membe (Mb) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Tuzo
iliyotolewa na Rais Mugabe kwa Brig. Jen. Hashim Mbita wakati wa Mkutano
wa Wakuu wa Nchi wa SADC uliofanyika Victoria Falls nchini Zimbabwe
mwezi Agosti 2014. Waziri Membe alieleza kuwa Rais Mugabe alitoa Tuzo ya
Munhumutapa kwa Brig. Jen Hashim Mbita kutokana na mchango wake mkubwa
katika harakati za kutafuta uhuru Kusini mwa Afrika. Brig. Jen. Mbita
anakuwa mtu wa kwanza sio Mkuu wa Nchi kutunukiwa Tuzo hiyo ambayo kwa
kawaida hutukiwa Wakuu wa Nchi pekee. Wengine katika picha ni Balozi wa
Zimbawe nchini Tanzania na binti yake Brig. Jen. Mbita, Bibi Shella.
Bibi Shella akitoa neno la shukrani kwa Serikali ya Zimbabwe kutokana na zawadi ya Dola 100,000.00 kwa Baba yake mzazi
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Shiyo Innocent (tai
nyekundu) na Afisa wa Ubalozi wa Zimbabwe nchini Tanzania wakifuatilia
kwa makini mkutano wa waandishi wa habari
Waandishi wa habari wakiwa kazini
0 comments: