MSANII AIBUA TIMBWILI KANISANI NI SIKU YA MAZISHI YA MTOTO WA MZEE MAGARI
Mauzauza? Katika
hali ya kushangaza, mwigizaji wa Kundi la Vituko Show linalorusha
vipindi vyake kwenye Runinga ya Channel Ten, Jasmini Emiry anadaiwa
kuzua timbwili kanisani na kusababisha tafrani madhabauni ikisemekana ni
mapepo.
Mwigizaji
wa Kundi la Vituko Show linalorusha vipindi vyake kwenye Runinga ya
Channel Ten, Jasmini Emiry akiwa katika hali ya sintofahamu.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na
mwanahabari wetu lilijiri kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Patriki mjini
hapa, mwishoni mwa wiki iliyopita, wakati wa kuaga mwili wa msanii
mwenzake, Shirley Edward almaarufu Sherry Magali.
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movies wakichukua uamuzi wa kumtoa nje ya kanisa ili ibada ya mazishi iendelee.
Awali, kabla ya zoezi la kuaga mwili wa
marehemu, Jasmini, akiwa benchi la mwisho nyuma sambamba na wasanii
wenzake akiwemo Asha Boko na mke wa Mzee Majuto, Rehema Majuto,
alionekana mwenye simanzi kupita kiasi.
Ulipofika muda wa kuaga, Jasmini
alipomaliza kulizunguka jeneza lililobeba mwili wa Sherry mbele ya
madhabahu, alianguka na kuanza kurusha mateke kama punda huku
akizungumza maneno yasiyoeleweka.
Baada ya kuona hivyo, baadhi ya wasanii
wa Bongo Movies mjini hapa wakiongozwa na Chediel Senzighe walimbeba
msanii huyo na kumtoa nje huku akiwapiga na kuzua tafrani ya aina yake.
Alipofikishwa nje, Jasmini alilala
kwenye tairi la gari Toyota Coaster akitaka limkanyage afe na alipotoka
hapo alikimbilia ofisini kwa paroko na kujilaza kwenye kiti ambapo
wasanii wenzake walimkamata na kuondoka naye kwenye Coaster kisha kwenda
kuzika Makaburi ya Kola mjini hapa.
0 comments: