BOB JUNIOR AFUMWA LIVE NA ‘MCHEPUKO’

Mchepuko? Baada ya kuachana na mkewe, Halima Ally, staa wa Nyota ya Chipsi Mayai na Prodyuza wa Sharobaro Records, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior’ amenaswa live na mrembo anayejulikana kwa jina la Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ ambaye ni msanii wa filamu, wakiwa katika mahaba nipoteze
kama ndege ya Malaysia.
Staa wa Nyota ya Chipsi Mayai , ‘Bob Junior’ akiangusha busu shavuni mwa mrembo anayejulikana kwa jina la Sabrina Omary ‘Sabby Angel’
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Sabby ambaye ndiye aliyevujisha picha za tukio hilo, Sabby na Bob Junior kwa sasa wako katika mahaba mazito na ni watu wanaopendana kwa sababu kila unapomuona Sabby yupo karibu na mwanamuziki huyo.
Bebi huyo, ‘Sabby Angel’ akimkubatia 'Bob Junior' kimahaba.
“Sasa hivi Sabby na Raheem ndiyo habari ya mjini kwani kila sehemu wapo pamoja na wanapendana sana,” alidai rafiki huyo wa Sabby.Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kwamba wawili hao wanaweza kuvalishana pete ya uchumba muda wowote kuanzia sasa.
Kwa pamoja 'Bob Junior' na mtoto ‘Sabby Angel’ wakidendeka bila dalili zozote za uoga.
Baada ya kunyetishiwa ubuyu huo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Bob Junior ambaye hakupatikana lakini alipotafutwa Sabby ili kusikia kauli yake kuhusu uhusiano wake na Bob Junior alikiri na kusema kuwa ni mtu ambaye anampenda na ndiye anamfanya awe na furaha.

0 comments: