SHEHE: AUNT EZEKIEL HANA NDOA
SHEIKH Mkuu
wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa ameweka wazi kuwa msanii nyota wa
filamu, Aunt Ezekiel ambaye aliolewa na Sunday Demonte hana ndoa
kutokana na kukaa mbali na mumewe kwa zaidi ya miezi sita.
“Hakuna ndoa kati ya mtu yeyote ambaye amezidi miezi 6 bila kukutana na mumewe kwa mujibu wa dini ya kiislamu.
“Kwa kawaida mwanamke ambaye hajakutana na mumewe kwa miezi 6 au zaidi
baada ya ndoa yao, hupaswa kwenda mara moja Baraza Kuu la
Waislamu Tanzania (Bakwata)
kulalamika na hatimaye kudai talaka, ikiwa mwanamke ameridhika na hali
hiyo, naye akaamua kukaa kimya huku akifanya mambo yake na kuanzisha
uhusiano na wanaume wengine maana yake amejitoa mwenyewe kwenye mamlaka
ya mumewe, hivyo hapo kunakuwa hakuna ndoa tena,”alisema Shehe.
0 comments: