T.I amehojiwa tena Marekani na kuzungumzia mengine mapya kuhusu Tanzania T.I

T.IClifford Joseph Harris, Jr. a.k.a T.I mkali kutoka Marekani aliyeangusha show ya nguvu katika
jukwaa la Fiesta 2014 siku ya Jumamosi Oktoba 18 2014 katika viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam, bado ameendelea kuyasimulia mazuri
na makubwa ya kuvutia aliyokutana nayo Tanzania.
Katika mahojiano aliyofanya New York Marekani na kituo maarufu cha redio Power 105.1kwenye show ya Breakfast Club, T.I amesema tangu aanze kufanya muziki hajawahi kufanya show kwenye jukwaa lolote mbele ya mashabiki zaidi ya 50,000.
T.I amelinganisha idadi hiyo kubwa aliyokutana nayo Tanzania kuwa ni sawa na kufanya show katika uwanja wa mpira wa miguu na kuujaza kwa show moja, kitu ambacho anakiona kabisa sio rahisi na ndio maana hii ya Leaders imekua kubwa kwake.
Swali la kuhusu Ebola bado liliulizwa kwa T.I kama alichukua tahadhari kwa kufanya utafiti kabla ya kwenda Afrika na kusema hakuwa na hofu yoyote alipokuja Tanzania, zaidi alikuwa akifikiria tu kuhusu mpenzi wake, hata hivyo hakukutana na Ebola wala kuona hata dalili za uwepo wake na kusisitiza kwamba mara nyingi Ebola imekua ikiwapata Wanaowahudumia wagonjwa’
Kwenye sentensi nyingine rapper huyu mwenye umri wa miaka 34 alisifia jinsi alivyopokelewa vizuri na kusema Tanzania ni watu wazuri hivyo akamwambia Dj Envy kwamba ataenjoy sana kwenye safari yake ya Afrika December mwaka huu.
Video ya T.I akiwa katika mahojiano hayo nimeshare na wewe mtu wangu wa nguvu, unaweza kuitazama hapa.

0 comments: