UKATILI...!! KIKONGWE WA MIAKA 81 ABAKWA HUKO MBEYA,WABAKAJI WAONDOKA NA DAMU YA SEHEMU ZA SIRI...
MKAZI
wa kijiji cha Luteba, wilayani Rungwe mkoani Mbeya, jina linahifadhiwa
(81) amedaiwa kubakwa na watu wasiojulikana na kumsababishia maumivu
makali.
Akisimulia
mkasa huo Bibi huyo, alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku
majira ya saa 8:00 wakati bibi huyo akiwa amelala nyumbani kwake, ambapo
alisikia kishindo cha watu ambao walimvamia na kumfunga kitambaa usoni
na kuanza kumuingilia kimwili.
Niliwaambia niwape hela wakasema hawana shida na kuniambia nikipiga kelele wataniua na ndipo walipoanza kunivua nguo kinguvu na kufanikiwa kunitendea unyama huo na na kuondoka na damu iliyokuwa ikinitoka
alisema
Alisema walipoondoka aliamua kupiga kelele za kuomba msaada kwa majirani waliompeleka katika kituo cha afya.
Mganga
Mkuu wa kituo hicho Dk. Edwin Mwakisisya, alikiri kumpokea Bibi huyo na
kudai kuwa wanaendelea kumfanyia matibabu kwa lengo la kumrudisha
katika hali yake ya kawaida.
Akizungumza
kwa niaba ya wazee wa makanisa wilayani humo mzee wa kanisa la Baptist,
Syemi Melele, alisema vitendo hivyo vimekuwa vikijitokeza mara kadhaa
na kwamba wanajipanga kuitisha makongamano yatakayoendana na maombi kwa
jamii hiyo ili iache vitendo hivyo.
Jeshi la polisi wilayani humo linaendele na uchunguzi wa kuwabaini wahusika wa tukio hilo.
0 comments: