MWANA CCM ATEKWA, AUAWA
UKATILI!
Watu wasiojulikana wameyakatisha maisha ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya
Chama cha Mapinduzi (CCM), Tawi la Mkwajuni, Kigamboni jijini Dar,
Ibrahim Hamis (30).Tukio hilo la kusikitisha na lililowaacha midomo wazi
wakazi wa eneo hilo, lilijiri usiku wa saa mbili hivi karibuni.
Waombolezaji
wakiubeba mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha
Mapinduzi (CCM), Tawi la Mkwajuni, Kigamboni jijini Dar, marehemu
Ibrahim Hamis (30).
Akizungumza na waandishi wetu mwishoni
mwa wiki iliyopita, mmoja wa viongozi wa chama hicho kutoka Shina Namba
13 Mkwajuni Vijibweni, Mrisho Bindo alisema siku ya tukio, marehemu
alikuwa kwenye pikipiki akimpeleka mtu mahali.
Alisema baada ya kumfikisha mtu huyo
eneo linaloitwa Mkorea, akiwa anarudi alitekwa na watu wasiojulikana
na kumpotezea uhai kwa kumteka na kumuua kwa kumpiga na kitu kizito
kichwani kisha kuchukua pikipiki yake na kutokomea kusikojulikana.
Bindo ambaye ni mjumbe wa shina huko
Kigamboni aliongeza kuwa eneo alilofanyiwa ukatili marehemu lina hali
mbaya kiusalama maana ni porini hasa kwa nyakati za usiku ni tatizo kwa
wapita kwa miguu.
Katika msiba huo, diwani wa eneo hilo kupitia CCM, Suleiman Methew Luwongo alilaani vikali mauaji hayo ambayo yamekatisha uhai wa kiongozi huyo na kuiacha familia yake ikiwa haina cha kufanya.
Katika msiba huo, diwani wa eneo hilo kupitia CCM, Suleiman Methew Luwongo alilaani vikali mauaji hayo ambayo yamekatisha uhai wa kiongozi huyo na kuiacha familia yake ikiwa haina cha kufanya.
Aidha, aliomba eneo hilo ambalo hadi
sasa limekaa kama pori wagawiwe watu ili waweze kuliendeleza kuliko
maeneo hayo kutumika katika uporaji na mauaji kwa watu.‘’Ninaiomba
serikali kupitia wizara husika kulifanyia utaratibu lile eneo ikiwa ni
kulimilikisha kwa wakazi wa huko ili liendelezwe,’’ alisema kiongozi
huyo.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Temeke, ACP Kihenya wa Kihenya alitihibitisha kutokea kwa tukio hilo
na akasema zoezi la kuwasaka watuhumiwa linaendelea.Marehemu alizikwa
Oktoba 12, mwaka huu katika Makaburi ya Vijibweni, Kigamboni jijini Dar
es Salaam.
0 comments: