UNAAMBIWA WEMA SEPETU AZUA KIZAAZAA HUKO KWENYE GEREZA LA CHINA
KUONESHA ameguswa, Beautiful Onyinye, Wema Sepetu ‘Madam’ alizua kizaazaa cha aina yake alipomtembelea mwanamitindo Jacqueline Fitizpatrick Cliff ‘Jack Patrick’ gerezani nchini China.
Tukio hilo lilitokea juzikati kwenye gereza lililopo Mji wa Macau ambapo Wema aliambatana na meneja wake, Martin Kadinda pamoja na shemeji yake, Petit Man.
Tukio hilo lilitokea juzikati kwenye gereza lililopo Mji wa Macau ambapo Wema aliambatana na meneja wake, Martin Kadinda pamoja na shemeji yake, Petit Man.
Chanzo kilicho
karibu na Wema kimeeleza kuwa, Wema alipofika na kuona mazingira ya
upweke ambayo Jack anaishi, aliwaza kwa muda na kuzungumza maneno kama
mtu aliyechanganyikiwa hivyo kuwatia hofu Martin na Petit.
Mwanamitindo Jacqueline Fitizpatrick Cliff ‘Jack Patrick’ wakati akiwa huru Bongo.
“Ilikuwa
mshikemshike, alimmis sana Jack sasa alipomuona na mazingira yale ya
upweke ndicho kilichomchanganya Wema lakini baadaye kina Martin
walimrudisha kimawazo na hatimaye akawa sawa,” kilisema chanzo hicho na
kuongeza:
Kete za madawa ya kulevya zilizowahi kunaswa.
“Hata
hivyo, Wema amesema mazingira ya kule ndani siyo mabaya lakini
kilichomuumiza yeye ni upweke ambao anao na watu wanaomzunguka.”Jack alikamatwa Desemba 19, mwaka jana akiwa amebeba madawa ya kulevAAya aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 1.1 katika Uwanja wa Ndege wa Macau akitokea jijini Bangkok nchini Thailand kuelekea Guangzhou, Mji Mkuu wa JAimbo la Guangdong Kusini mwa China.
Agosti, mwaka huu Jack Patrick ilielezwa kuwa alihukumiwa kifungo cha miaka sita jela huku kukiwa na uwezekano wa kupunguziwa adhabu endapo ataonesha utiifu gerezani.
0 comments: