WANANCHI WACHOMA BUNGE MOTO KUPINGA KUPITISHWA KWA KATIBA
Waandamanaji hao wakishangilia baada ya kuchoma bunge.
Magari nayo yameteketezwa kwa moto.
WAANDAMANAJI nchini Burkina Faso leo
wamechoma moto bunge la nchi hiyo kupinga kupitishwa kwa katiba
itakayomruhusu rais wa nchi hiyo, Blaise Compaore kuongeza muda wa kukaa
madarakani.
Rais Compaore anataka kuongeza muda zaidi katika utawala wake wa miaka 27 aliyotumia kuliongoza taifa hilo.
Taarifa kutoka Mji Kuu ya nchi hiyo,
Ouagadougou, zinasema kuwa ukumbi wa chama tawala na makao makuu ya
chama hicho cha Congress for Democracy and Progress yamechomwa moto pia.
Bunge hilo lilitaka kubadili katiba
itakayomuwezesha Compaore, aliyeingia madarakani tangu mwaka 1987 ili
aweze kuiongoza tena nchi hiyo mwakani.
Kumekuwepo kampeni za wapinzani wanaomtaka rais huyo kuachia ngazi na kutogombea katika uchaguzi wa mwaka ujao.
Kabla ya kuchomwa moto bunge hilo,
polisi walilipua mabomu ya machozi kuwazuia waandamanaji waliokuwa
wakielekea katika jengo la bunge hilo japo takribani watu 1,500
walifanikiwa kupenya na kulichoma bunge hilo.
Waandamanaji walionekana wakichoma
nyaraka na kupora baadhi ya vifaa vya kompyuta huku magari yaliyokuwa
nje ya jengo hilo nayo yakichomwa moto.
0 comments: