AIBU:NJEMBA ADAIWA KURUBUNI WAKE ZA WATU KINGONO ANASWA
Mji wa Morogoro umekumbwa na matukio
mfululizo ya mafumanizi ambapo baada ya ticha wa shule ya msingi
kufumaniwa na dereva wa bodaboda kisha jamaa kubondwa kwa kukutwa
akifanya ngono na mke wa mtu vichakani na denti wa upadri kufumaniwa,
mwanzoni mwa wiki hii fumanizi lingine kiboko la njemba mwenye asili ya
Kiarabu limetokea.
Wakinamama (kushoto) wakimficha mwenzao (mke wa mtu) aliyenaswa kwenye ghetto la njemba mwenye asili ya Kiarabu, Hemed.
Kwenye Kata ya Mazimbu mjini hapa
mwanaume aliyefahamika kwa jina moja la Hemed, anadaiwa kunaswa laivu na
mke wa mtu kwenye chumba anachoishi kilichopo Mtaa wa Boma mjini hapa.
Ikiwa kazini, Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers ilinyetishiwa kuwepo kwa ishu hiyo hivyo kufika eneo la tukio ndani ya dakika sifuri na kunasa tukio hilo likiwa bichi.
Ikiwa kazini, Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers ilinyetishiwa kuwepo kwa ishu hiyo hivyo kufika eneo la tukio ndani ya dakika sifuri na kunasa tukio hilo likiwa bichi.
Katika fumanizi hilo lililojaza ‘inzi’
(umati), Hemed alidaiwa kuwa amekuwa na tabia ya kuwarubuni na kumwaga
fedha mbuzi kwa wake za watu na kuserebuka nao ndani ya ‘geto’ lake
jambo lililowafanya wenye wake zao kumwekea mtego ambao ulipofyatuka
ukamnasa majira ya saa 3:00 asubuhi.
Akihojiwa na gazeti hili, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisema kuwa, jamaa huyo alikuwa na mwanamke mzuri wa umbo aliyetajwa kwa jina moja la Husna ambaye alikutwa chumbani kwa Hemed.
Akihojiwa na gazeti hili, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisema kuwa, jamaa huyo alikuwa na mwanamke mzuri wa umbo aliyetajwa kwa jina moja la Husna ambaye alikutwa chumbani kwa Hemed.
Akizungumza na mwanahabari wetu kwenye
eneo la tukio, mume wa Husna aliyejitambulisha kwa jina moja la Siri
alikuwa na haya ya kusema:
“Nilimuaga mke wangu nakwenda Mwanza kwenye shughuli zangu za biashara. Nikiwa Mwanza nilijulishwa na majirani kwamba mke wangu kila siku anaacha watoto wetu kwa mama yake na kwenda kulala kwa Mwarabu.

“Ukweli kama mwanaume nilipatwa na hasira, nikatafuta ndege nikarudi hapa (Morogoro).
“Nimeelekezwa kwa Mwarabu na jamaa waliokuwa wamemwekea mtego, nilipofika nilichungulia dirishani, nikamuona mke wangu na Mwarabu wakiwa kitandani.
“Nilihisi kupooza mwili na roho ilikuwa inaniuma sana.”

Aliongeza: “Mimi na mke wangu tumefunga
ndoa ya Kiislamu, tuna watoto wawili, mmoja ana umri wa miaka mitano na
wa pili ana mwaka mmoja na miezi saba.
“Cha ajabu mtoto wa pili hadi sasa hatembei. Kwa tukio kama hili nahisi mke wangu amembembenda.”
“Cha ajabu mtoto wa pili hadi sasa hatembei. Kwa tukio kama hili nahisi mke wangu amembembenda.”
Kwa upande wake Husna ambaye alisitiriwa
na wanawake wenzake waliokuwa wakimficha, alipotakiwa kuzungumzia tukio
hilo, alimjia juu mwanahabari wetu na kumtolea maneno ya shombo.
Naye Mwarabu huyo alipohojiwa, pia alimtolea vitisho ‘kamanda’ wetu.
Kufuatia wingi wa watu, wawili hao walifungiwa chumbani lakini raia wenye hasira kali wakavunja mlango na kuwashushia kichapo.
Kufuatia wingi wa watu, wawili hao walifungiwa chumbani lakini raia wenye hasira kali wakavunja mlango na kuwashushia kichapo.
Baadaye viongozi wa Kata ya Mazimbu
wakiongozwa na Afisa Mtendaji, Brioht Sospeter na polisi mmoja walifika
eneo la tukio wakawaondoa wawili hao na kuwapeleka ofisi ya kata kwa
mahojiano zaidi.
0 comments: