ESTER KIAMA: BILA MILIONI 5 SIJAOELEWA

Kwenye kiwanda cha filamu Bongo sasa kuna warembo wakali wanaotishia amani wakongwe. Waswahili wanasema, hawavumi sana lakini ni moto wa kuotea mbali kwa uigizaji na muonekano pia.
Safu hii wiki hii imebahatika kumnasa mwanadada anayekwenda kwa jina la Ester Kiama. Amebanwa kwa maswali 10 ambapo bila hiyana alitoa ushirikiano. Ungana na mwandishi wetu Imelda Mtema aliyefanya naye mahojiano.
Muigizaji wa filamu Bongo, Ester Kiama.
Ijumaa: Wewe ni binti mrembo sana, unakabiliana vipi na hii rushwa ya ngono ambayo inaonekana kuwatesa mabinti wengi wanaochipukia?Ester: Nimeingia kwenye fani nikijua vitu hivyo vipo, kikubwa ni mimi kujiheshimu na kutotengeza mazingira ya wanaume wakware kunichukulia poa.
Ijumaa: Kila kukicha kwenye filamu wanawake mastaa wamekuwa wakiingia kwenye mabifu huku tabia ya kuchukuliana mabwana ikionekana kushika kasi, hali hii wewe unaizungumziaje?Ester: Kusema ukweli nakereka sana na hii tabia ya kuchukuliana wanaume na kimsingi haya mabifu tusipokuwa makini nayo yanaweza kuturudisha nyuma badala ya kwenda mbele.
Ijumaa: Je, una mpenzi?
Ester: Ninaye na kwa kweli nampenda sana kiasi kwamba siku nikisikia mtu anammendea, mbona atanitambua.
Ijumaa: Inadaiwa kuna pedeshee mume wa mtu ambaye anakuhudumia, hebu funguka juu ya hili.
Ester: Kama nilivyosema, mpenzi ninaye, siwezi tu kumuanika kwa sasa ila siyo pedeshee na wala sina taarifa kuwa ana mke, najua ni wangu pekee.
Muigizaji wa filamu Bongo, Ester Kiama akiwa kazini.
Ijumaa: Vipi kuhusu hii tabia ya usagaji, ulishawahi kutokewa na staa yeyote akitaka mfanye hako kamchezo?
Ester: Najua hako katabia kapo ila mimi hajawahi kunitongoza mwanamke yeyote, akitokea wa kuniambia maneno hayo nitamchukia milele.
Ijumaa: Ni staa gani wa kiume anayekuvutia?
Ester: Anayenivutia ni Ray ila naomba watu wasinifikirie tofauti, ananivutia kwa uigizaji wake na siyo mambo mengine.
Ijumaa: Kwa mfano umebahatika kupata mchumba, ukiambiwa utaje mahari yako utataja kiasi gani?
Ester: Mimi ni mwanamke mzuri, najiamini na hivyo atakayetaka kuniweka ndani ajiandae mahari ya shilingi milioni 5.
Ijumaa: Ni sehemu gani ya mwili wako unaipenda zaidi?
Ester: Makalio yangu, kiuno changu na miguu yangu. Yaani kwa kifupi kuanzia kiunoni kushuka chini.
Ijumaa: Kuna kamtindo ka’ baadhi ya mastaa wanapotoka ‘out’ hasa nyakati za usiku kutopenda kuvaa makufuli, kwako wewe vipi?
Muigizaji wa filamu Bongo, Ester Kiama akiwa na wasanii wengine wa maigizo.
Ester: Yaani mimi nisipovaa kufuli najiona kama vile natembea mtupu. Siyo tabia nzuri hata kama wanadai eti zinachubua lakini siyo ustaarabu.
Ijumaa: Kuna filamu ambayo umecheza mpya?
Ester: Ndiyo, inaitwa Mikononi Mwa Polisi, naamini kwenye filamu hiyo watu watakijua vizuri kipaji changu.

0 comments: