CHID BENZ NA FID Q WAFANYA ALBUM YA PAMOJA

Wakali wa Hip Hop Tanzania Rashid na Fareed a.k.a Chid Benz na Fid Q wana mpango wa kurekodi album ya pamoja.



Chid ambaye ameachia ngoma mpya wiki hii ‘Kimbiza’, ameiambia 255 ya XXL ya Clouds Fm kuwa mpango wa kufanya album na Fid lilikuwa ni wazo lake.

“Ni idea yangu nilikuwa nayo kabla sijatoa ngoma, sikujua kama nitakuja kuwa busy na ngoma kwahiyo nilikuwa najua kwamba kwa kipindi ambacho nitakuwa nimekaa nirekodi project na Fid, so imekuja imekuwa”.

“Mpaka sasa hivi sijarekodi lakini tupo kwenye project yetu ya mimi na Fid, kwahiyo soon tutaanza kuirekodi kwasababu tulisharekodi ngoma moja so nafikiri sasa now tunatakiwa tuingie mzigoni, so nahisi the project itakuwa noma…” 



Aliongeza,“mi najitayarisha kuingiaingia vistudio napitia vistudio viwili vitatu hapa na pale, kwahiyo natafuta bado nahisi nikija kupata msumari ntakuja tu kusema jamani eeh baada ya huu ni huu…tunafanya album nzima inabidi tupige mikono tu Chid na Fid kwasababu ni Rashid na Fareed, kwahiyo tumeamua sisi wenyewe kufanya kwasababu kila siku tunakaa tunazungumza tunacheka tunatania kila siku tuko busy na music lakini tunaweza tukapata nafasi tukafanya kitu so tumeamua tufanye album tupige mikono ya ajabu.

0 comments: