AIBU!! BABY MADAHA, ISABELA WAFANYA UFUSKA!
HAMNAZO? Mastaa
wa Bongo Fleva, Isabela Mpanda ‘Bella’ na Baby Madaha wamenaswa
wakifanya vitendo vichafu maeneo ya Tabata jijini Dar baada ya kupiga
masanga ya kutosha mwilini.
Kwa mujibu wa chanzo, Baby na Bella
walifika maeneo hayo juzikati wakiwa wazima kabisa lakini baada ya
kufakamia pombe kwa kasi ndipo walipoanza kufanya madudu huku mchumba wa
Bella, Luteni Kalama, akiwakimbia na kuwaacha wenyewe.
“Walianza kushikanashikana kama
wanasagana, wakapakatana huku wakiwa na chupa za pombe wakicheza kwa
hisia za kimahaba kama mtu na mtuwe, yani Kalama anatakiwa ajiongeze
vinginevyo mkewe mtarajiwa ataharibikiwa,” kilisema chanzo.
Baada ya paparazi wetu kunasa picha tukio hilo kutoka kwa sosi, aliwavutia
waya wawili hao kwa nyakati tofauti
ambapo walisema hawaoni tatizo katika mambo hayo
waliyoyafanya.“Tulikunywa pombe zetu na hatukuwa na tatizo na mtu yeyote
kuna shida gani? Hakuna vitendo vibaya tulivyofanya kwa sababu
hatukugombana na tulikuwa tuko na amani na raha zetu,” alisema Baby
huku Bella naye akitoa maneno yanayofanana kabisa na hayo ya Baby.
0 comments: