HOFU YATANDA,MSHITUKO WA VIFO VYA WASANII... NDANI YA MASAA 24 WAFARIKI DUNIA WANNE
Misiba
kila kona! Achilia mbali watu wasiokuwa na majina hasa vijana wadogo,
ndani ya saa 24 wamefariki dunia wasanii wanne wa kutoka kwenye tasnia
za Bongo Movies na Bongo Fleva, Amani lina habari yenye kuumiza moyo.
Benson
Okumu, enzi za uhai wake akiwa na mtoto wa marehemu George Okumu Otieno
‘Tyson’ , Sonia. HAWA HAPA Matukio hayo yalitokea kati ya Jumatatu
jioni na Jumanne asubuhi ambapo kutoka kwenye tasnia ya filamu
waliotangulia mbele ya haki ni pamoja na Sherry Salum ‘Sheri Magali’,
Arafa na Benson Okumu Otieno. Kwa upande wa Bongo Fleva, Yessaya
Ambikile ‘YP’, naye alitangulia mbele ya haki ikiwa ni siku chache tu
alionekana kwenye kumbi mbalimbali jijini Dar. ALIANZA MDOGO TYSON
Jumanne jioni, gazeti hili lilipokea kwa masikitiko kifo cha mdogo wa
marehemu George Okumu Otieno ‘Tyson’ aitwaye Benson Okumu Otieno ‘Benii’
ambaye alifariki dunia baada ya kupata homa kali na kuchanganyikiwa.
Marehemu YP |
Marehemu
YP kutoka Kundi la TMK Wanaume Family enzi za uhai wake. Babari za
ndani zilieleza kwamba Benii alianza kuumwa mkono kawaida ambapo
alitumia dawa lakini baada ya siku chache mkono huo ulianza kuvimba na
kupata homa kali iliyosababisha kwenda hospitali. Ilielezwa kwamba Benii
alikwenda Hospitali ya Lugalo, Dar ambapo homa ile ilipanda kichwani na
kumfanya achanganyikiwe, mwisho akaaga dunia. Baada ya msiba huo
kutokea, taratibu za kuusafirisha mwili kwenda kijijini kwao Kisumu
nchini Kenya zilifanywa nyumbani kwa mdogo wake wa kike maeneo ya
Sinza-White Inn jijini Dar. Habari zilieleza kwamba Benii alikuwa
akifanya kazi za uongozaji wa filamu (director) ambapo alifanikiwa
kufanya filamu na wasanii mbalimbali. Benii alianza kazi hiyo alipofika
jijini Dar akiwa anaishi na kaka yake, George Tyson aliyefariki dunia
Mei 30, mwaka huu kwa ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Gairo mkoani
Morogoro.
Marehemu Arafa
aliyekuwa msanii chipukizi ndani ya Bongo Movies enzi za uhai wake.
“Jamani tatizo ni nini? Hata maumivu ya kifo cha kaka yake hajaisha,
jamani na Benii naye? Tumuombe sana Mungu atuepushe na balaa hili la
vifo,” alisema mwigizaji mkubwa Bongo, William Mtitu. ARAFA WA BONGO
MUVI AFIA INDIA! Huku na huku, wakati watu wakitafakari kifo cha Benii
na taratibu za kuusafirisha mwili wake, ghafla ziliibuka habari nyingine
mbaya kuwa chipukizi wa Bongo Movies aliyetajwa kwa jina moja la Arafa
naye aliaga dunia jioni hiyo ya Jumatatu. Habari zilieleza kwamba Arafa,
mtoto mzuri mwenye mvuto huku akiwa na umri chini ya miaka 20, anadaiwa
kupelekwa nchini India na mama mmoja kwa shughuli binafsi.Ilielezwa
kwamba, akiwa nchini humo aliumwa ghafla (ugonjwa haukutajwa) ndipo
akapoteza uhai hivyo taratibu za kuurejesha mwili wake Bongo
zinaendelea.
Marehemu Sherry Magali wa Bongo Movies enzi za uhai wake |
Marehemu Sherry Magali wa Bongo Movies enzi za uhai wake |
. YP NAYE AAGA
DUNIA Msanii YP kutoka Kundi la TMK Wanaume Family, naye aliaga dunia
usiku wa kuamkia Jumanne wiki hii. Habari kutoka kwa familia yake
zilieleza kwamba YP alianza kusumbuliwa na kifua tangu mwezi Machi,
mwaka huu ambapo alitibiwa na kuanza dozi. Kwa mujibu wa mkewe, Sakina
Robert na dada yake Hawa Ambikile, YP alimaliza dozi mwezi Septemba,
mwaka huu ambapo hivi karibuni hali ilibadilika na kuwa mbaya
zaidi.Mkewe alisema alikimbizwa katika Hospitali ya Temeke, Dar ambako
alipatiwa matibabu hadi umauti. Meneja wa TMK Wanaume Family, Said Fela
alisema msiba wa msanii huyo uliwekwa Keko, Dar nyumbani kwa baba yake
na alitarajiwa kuzikwa jana saa 10:00 jioni kwenye Makaburi ya
Chang’ombe jijini Dar. Fela alisema kuwa YP alifanya vizuri kimuziki
wakati na msanii mwingine Y Dash ambapo alisikika kwenye ngoma kibao
kama Ulipenda Pesa na Pumzika. MASKINI! ALIPANGA KUACHIA NGOMA MPYA
Ngoma nyingine nyingi alifanya na TMK Wanaume Family kama Twende Zetu ya
Chegge Chigunda, Dar Mpaka Moro, Kichwa Kinauma na Tufurahi na tayari
alikuwa amerekodi wimbo wake mpya akiwashirikisha Tip Top Connection
unaokwenda kwa jina la Wazee wa Jiji aliopanga kuuachia mwezi ujao. YP
ameacha mke na mtoto mmoja wa kike mwenye umri wa miaka saba. BURIANI
SHERRY MAGALI! Wakati pigo la TMK Wanaume Family likiumiza, majira ya
saa 6:00 mchana, siku ya Jumanne iliyopita, ghafla kuliibuka habari
nyingine mbaya kwenye Bongo Movies baada ya kuondokewa na mwigizaji
ambaye ni mchekeshaji, Sherry Magali. Sherry Magali aliaga dunia wakati
akipatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro baada
ya kusumbuliwa na maradhi ya kifua na moyo kwa muda mrefu. Jumamosi
iliyopita mwanahabari wetu alimtembelea wodi namba nane ambapo Sherry
Magali alisimulia namna alivyokuwa akipata maumivi makali nay a muda
mrefu tangu mwaka jana huku akionekana kudhoofu mwili na kukosa nguvu.
Baada ya kukutwa na umauti, msiba uliwekwa nyumbani kwao maeneo ya Mji
Mpya mjini hapa kwa mzee Msafiri Ngedele. Mazishi ya Sherry yalitarajiwa
kufanyika jana kwenye makaburi ya Kola mjini hapa. Enzi za uzima wake,
Sherry Magali alisifika kwa kuchekesha na lile umbo lake zuri lililokuwa
likiwatoa midume udenda.Mungu azilaze roho za marehemu wote mahali pema
peponi-Mhariri. Imeandaliwa na Hamida Hassan, Chande Abdallah,
Deogratius Mongela, Shani Ramadhan, Gladness Mallya na Dustan Shekidele,
Morogoro.
0 comments: