MAIMARTHA :NAKERWA NA MASTAA WA KIKE WA BONGO MUVI WANOTOKA KIMAPENZI NA VIJANA WADOGO "SERENGETI BOY"
Mtangazaji ambaye pia ni mjasiriamali,
Maimartha Jesse amewaponda mastaa wa Bongo Muvi wanaotoka kimapenzi na
vijana wadogo ‘Serengeti Boys’ akidai kuwa wanajichoresha.
Akipiga stori na Ijumaa hivi karibuni,
Mai alisema anawashangaa baadhi ya mastaa hao kutoona aibu kutangaza
kuwa wanatoka na Serengeti Boy huku wakionekana maeneo mbalimbali
wakiponda raha.
“Mimi mpaka naogopa na nawaonea huruma
kwani hali ni mbaya jamani, watoto wadogo wanatoka na wasanii
waliowazidi sana kiumri, yani imekuwa ni kama fasheni sasa, huku ni
kujichoresha,” alisema Mai.
0 comments: