KUTANA NA NABII YASPI AWAPONYA WAGONJWA KWA KUTUMIA PAFYUMU DAR


Nabii Yaspi akiibariki moja ya pafyumu hizo.Hapa akiwapulizia wagonjwa mbalimbali.
NABII wa Kanisa la The Revelation Church lililopo Buza-Kipera jijini Dar,Yaspi Paul Bendera, amefanya miujiza ya aina yake kwa kuwatibu watu kwa kutumia pafyumu ambapo watu wenye magonjwa mbalimbali walidai kupona kwa kupuliziwa pafyumu hizo.
Tukio hilo lilijiri Jumapili ya Novemba 2 mwaka huu ambapo kwa mujibu wa Nabii Yaspi aliwaagiza wagonjwa wafike kanisani hapo na pafyumu kanisani hapo ili azibariki na kuwa dawa na kinga yao kwa magonjwa mbalimbali yanayowakabili1Ad Options

Waandishi wetu waliokuwa kanisani hapo walishuhudia umati wa wagonjwa wakiwa wamejipanga na pafyumu za kila aina na kuombewa kisha kunyunyiziwa marashi hayo na kudai kupona kabisa.

0 comments: