MSANII AFA AKITAJA JINA MAINDA
MSANII aliyefariki
dunia hivi karibuni mjini Morogoro, Sherry Magali, anadaiwa kuwa
alikuwa akilitaja jina la Ruth Suka ‘Mainda’ kila mara hadi alipofikwa
na umauti.
Chanzo chetu makini kilichokuwa karibu
na msanii huyo wa filamu, kinasema Sherry alianza kugoma kula akidai
hadi amuone msanii mwenzake huyo ambaye alikuwa jijini Dar es Salaam
anakoishi.
Mpashaji huyo alisema hata siku
aliyofariki pia alilitaja jina hilo, kitendo kilichowaumiza sana baadhi
ya ndugu na marafiki. Mainda ambaye alikuwa ni rafiki wa marehemu,
alikiri kusikia jambo hilo na anasikitika kwamba siku aliyopanga kwenda,
ndiyo ambayo mwenzake alifariki.
0 comments: