LADY JAYDEE NA MUMEWE GADNA KUPELEKANA KORTINI KISA KIPO HAPA......
Prizenta aliyetua Radio E-FM hivi karibuni akitokea Radio Times FM, Gardner G Habash ‘Kapteini’ anadaiwa kumpandisha kortini mkewe, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ kisa kikisemekana ni mgawanyo wa mali hivyo anataka haki yake baada ya kuwepo kwa madai mazito ya ndoa yao kuvunjika.
Kwa mujibu wa madai hayo, inasemekana kwamba Gardner amekimbilia mahakamani akidai apewe talaka na waweze kugawana mali walizochuma wote ili kila mmoja achukue hamsini zake.
Chanzo hicho ambacho ni mtu wa karibu wa familia hiyo kililiambia gazeti hili kwamba, siku chache baada ya kutengana na huku hali ikizidi kuwa mbaya, mtangazaji huyo alichukua hatua ya kutafuta msaada kwa wanasheria.
“Msinitaje jina ila ninachowaambia ni kwamba Gardner tayari ameshampata mwanasheria anataka kumshitaki Jaydee.
“Anachohitaji
ni kugawana mali zao, kila mtu afanye maisha yake na ukiangalia tu
Gardner hana mpango tena wa kuendelea na maisha ya ndoa na Jaydee ila
Jide yeye bado ana matumaini ya kurudiana wawe pamoja na hasa
kinachomuuma ni kugawana mali.
“Yaani Gardner ameshafanya kila aina ya jitihada ya kutaka waachane kiroho safi lakini
Jaydee anaonekana kutokubaliana na wazo hilo kwani anaogopa ule usemi
kwamba mwanamke mjinga huvunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe,”
kilisema chanzo hicho na kuongeza:“Ishu ya kugawana mali ya Gardner na
Jide ndiyo habari ya mjini na ili jamaa apate chake ameona heri atafute
mkono wa sheria.” Chanzo hicho kiliendelea kumwaga ‘ubuyu’ kwamba, kitendo cha Jaydee kutangaza kubadili mwelekeo wa mali zake akianza kwa kubadili jina la ule mgahawa wake kutoka lile la Nyumbani Lounge na kuuita M.O.G ndicho kimemshtua Gardner na watu wake wa karibu.
Kilendelea kudai kwamba, pia ishu ya Jaydee kubadili jina la Bendi ya Machozi na kuiita Lady Jaydee and the Band, nayo imemchochea Gardner na kuamua kukimbilia mahakamani.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, gazeti hili lilimtafuta Gardner ili aweke wazi madai ya kutaka kumburuza mahakamani mkewe huyo na haya ndiyo majibu yake mafupi: “Kaka kusema kweli hiyo ishu nashindwa kuizungumzia maana hata sijui wewe umeipata wapi dah.”
Gardner na Jaydee ambao walifunga ndoa mwaka 2005, wamekuwa wakidaiwa kuwa hawapo pamoja tena huku majukumu ya mtangazaji huyo ambaye alikuwa meneja wa mwanamuziki huyo yakichukuliwa na ndugu wa Jide ambaye ni msanii wa Bongo Fleva aitwaye Wakazi. >
0 comments: