PENNY: DIAMOND HANA CHAKE, NIMESHAPOSWA
MTANGAZAJI aliyewahi
kujiachia kimalovee na Nasibu Abdul ‘Diamond’, Penniel Mungilwa ‘Penny’
amesema mwanamuzi huyo kwa sasa alie tu kwani ameshachumbiwa na hawezi
kumpata tena.
Kauli ya mwanadada huyo ilikuja baada ya kuulizwa kama anaafikiana na
kauli ya mama wa Wema Sepetu, Miriam
Sepetu kwamba, kwa kuwa Wema kamuacha Diomond basi staa huyo wa Wimbo wa
Mdogomdogo bora akampose yeye.
“Mmh! Hapa suala la Diamond kurudiana na
mimi halipo kabisa maana simhitaji yeye wala mwanaume mwingine yeyote,
mimi ninaye wangu tayari ambaye ameshanichumbia hivyo sitarajii kabisa
kuwa na mwingine zaidi yake,” alisema Penny.
0 comments: