SHUGHULI YA NJEMBA ZENYE VIFUA VIPANA,NI HATARI KATIKA MAPENZI....!
Kuna mdahalo mkubwa ambao una majibu tofauti kuhusu wanaume wenye vifua vikubwa kama kweli wanapendwa sana na wanawake au la.
Unaweza
ukakutana na mwanadada akimsifia mkaka kwamba anakifua kizuri
akimaanisha kwamba ana kifua kipana ambacho kinajengwa kwa kufanya
mazoezi maalum, aina hii ya mwanamke bila shaka inaonesha kuwa
hupendelea zaidi wanaume wa aina hii na kwa hakika kama mume wake au
boyfriend wake atakuwa na kakifua kadogo hatapenda sana na wala
hataridhishwa na mwonekano wake kutokana na kupenda sana wanaume wenye
vifua kabati (vifua vikubwa).
Matokeo
yake ni kwamba ni rahisi zaidi kwa mwanamke huyu kushawishika na
wanaume wenye mafua makubwa kwani wewe mwenye kidogo sio mapenzi yake.
Kwa
upande mwingine usijeukashangazwa sana kukutana na mwanamke asiyetaka
hata kusikia kuhusu hawa wanaume wenye vifua vikubwa na huhisi hata
kichefuchefu kuona binadamu mwenye aina hii ya vifua. Hivyo kwa aina hii
ya mwanamke hakika kifua kikubwa (six packs) sio dili wala mpango
wowote na hata hawezi kushawishika na aina hii ya mwanaume,hivyo kwa
mwanamke huyu mwanaume mwenye kifua cha kawaida ndio humzimia zaidi na
huweza kuzuzuliwa kirahisi.
Hivyo
basi kama mwanaume jambo la msingi ni kuangalia aina gani ya kifua
mpenzi wako anapenda ndipo uamue kujenga kikubwa au kubaki hivyohivyo
japo kwa asilimia kubwa kwa wanawake wa kisasa ambao wanataka waonekane
kama wanakwenda na wakati hupendelea zaidi wanaume wenye vifua vikubwa
kama vya wacheza mieleka.
0 comments: