Stori kuhusiana na alichokisema Chris Brown kuhusu Rihanna,Drake pamoja na pepo linalomsumbua kwa sasa Chris & RiRi
Baada ya ukimya wa kama miaka 5 hivi, Chris Brown ameamua kuzungumzia yote yanayomhusu ikiwemo mahusiano yake na Rihanna.
Chris amesema kila kitu ni kama ilikuwa ‘mistake’, na hana haja ya kuwa
na majuto kwa kuwa tayari walirekebisha tofauti zao na kwa sasa ‘pepo’
alilonalo ni pepo la kuogopa kushindwa.
Akizungumzia kuhusu yeye na Rihanna, amesema “..naamini ilikuwa ni
makosa ambayo siwezi kuyarudia.. nikiangalia nilikuwa nna umri wa kama
miaka 17 au 18.. sasa nna 25.. najikuta bado natumikia adhabu ya kufanya
huduma za kijamii na natakiwa kuonana na jaji kila baada ya mwezi mmoja
na nusu kutokana na tatizo lile..”
Chris Brown na Rihanna walikaa kwenye headlines ambapo imesemekana
walijaribu kama kuufufua uhusiano wao, ambapo Chris anasema alihitaji
kumuonyesha Rihanna kwamba anaweza kubadilika na kuwa mwanaume ambaye
Rihanna anamuhitaji.
Baada ya Chris kumuona Rihanna kwenye show ya Oprah akizungumzia kwa
hisia kuhusu Chris, na kusema upo uwezekano wakawa marafiki, Chris
aliona namna ambavyo Rihanna anamjali, kitu ambacho hakuwahi kukiona kwa
kipindi kirefu, lakini kizaazaa kikawa pale Rihanna alipoanza ‘kutoka’
na Drake ambapo Chris alihisi kuwa Rihanna anafanya hivyo kumuumiza japo
yeye hana uadui na yoyote kati yao.
“.. Namna ninavyofanya.. Iko wazi.. Hii ni game, sisi ni vijana..
tunafanya hivi ni kwa sababu ya umri. Nadhani tukifikia miaka 30,
tutakuwa tumepevuka na malengo yetu hayatokuwa upande huo tena..”
“..Tumalizane na masuala ya ugomvi, itaonyesha namna gani tumekua na tumepevuka..”-Chris Brown
0 comments: