TIKO: JAPOKUWA ALIPA KIPIGO CHA NGUVU BADO NAMPENDA SIWEZI KUMUACHA
BAADA ya
mwanamuziki Tiko Hassan kupokea kipigo kutoka kwa bwana wake
aliyefahamika kwa jina moja la Ally, msanii huyo amesema hawezi kumuacha
kwani anampenda.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni,
Tiko alisema ni kweli ameumizwa kichwani lakini hawezi kufanya uamuzi wa
kumuacha kwa kuwa, anahisi kuna siku atajutia uamuzi wake huo.
“Ni kweli amenifanyia kitendo kibaya,
ameniumiza lakini najua ni hasira tu, hata yeye mwenyewe najua anajutia
hivyo siwezi kumuacha,” alisema Tiko ambaye alijiingiza kwenye filamu
lakini sasa kageukia muziki na anakuja na ngoma yake iitwayo Funga
Virago.
0 comments: