WALIMU WAKAMATWA WAKIFANYA MTIHANI WA FORM FOUR OFISINI
Licha ya walimu hao kukamatwa pia waliokuwa wasimamizi wa ndani wa mitihani kwenye shule hiyo, wameondolewa kutokana na uzembe.
Kaimu
ofisa elimu wa Wilaya ya Ngorongoro, Chacha Megewa alidai walimu hao,
Jakob Jadie na Reginald Boniface, walikamatwa wakati wakifanya mtihani
wa historia.
Alisema
walikamatwa Novemba 5 walikamatwa na msimamizi mkuu wa mitihani,
Faustine Bura baada ya kuingia ghafla katika ofisi ya mwalimu mkuu.
“Msimamizi alikuwa anafuata moja ya fomu ofisi ya mkuu wa shule, baadaye aliita polisi na kuwakamata,” alisema.
Kamanda
wa polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas jana hakupatikana kuelezea
tukio hili, lakini polisi Kituo kidogo cha Ngorongoro ilithibitisha
kukamatwa kwa walimu hao.
0 comments: