MAPYA YAIBUKA:MAMA KANUMBA AFICHUA MAZITO YA RAY, MWANAYE KANUMBA

BAADA ya hivi karibuni siri kufichuka kwamba Kundi la Bongo Movie linateswa na laana ya marehemu Steven Kanumba, mama yake Flora Mtegoa ameibuka na kueleza mazito yakiwemo ya aliyekuwa rafiki wa mwanaye, Vincent Kigos ‘Ray’, Risasi Jumamosi linakupa mchapo.
Mama yake marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa.
Akizungumza kwa hisia kali Mama Kanumba alisema anaungana na katibu msaidizi wa klabu hiyo, Devotha Mbaga kwamba kundi hilo lina laana ya Kanumba kwani naye kama mzazi ni shahidi kutokana na mwanaye kila wakati alikuwa akimfuata nyumbani akilia na kusema kwamba hawatakaa waelewane milele.
“Kanumba alikufa akiwa ameshajitoa Bongo Movie kutokana na majungu waliyokuwa wakimwandama kila kukicha na maneno yake ya siku chache kabla hajaaga dunia alikuwa akisema kwamba kundi hilo halitakaa lielewane milele kwa kuwa walikuwa wakimchukia na kumsemea majungu bila sababu hali iliyokuwa ikimsababisha kulia na kulalama kila wakati.
Aliyekuwa rafiki wa Kanumba, Vincent Kigos ‘Ray’.
“Alisema ukweli ni kwamba kundi hilo linakosa kuwa na maendeleo kwa sababu wanaendekeza majungu hivyo akaniambia mama nimejitoa huko japokuwa mimi ni mmoja wa waanzilishi yaani sitaki tena,” alisema Mama Kanumba.
Mama Kanumba alidai sababu ya ugomvi wa Ray na Kanumba ulitokana na kugombanishwa na Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ingawa siku chache kabla ya kifo cha Kanumba, familia zote mbili zilikaa na kusuluhisha ikawa imebaki kupeana mikono lakini Mungu hakupenda iwe hivyo, akamchukua Kanumba.
“Siwezi kusahau aliyewagombanisha Kanumba na rafiki yake wa damu Ray ni Steve Nyerere lakini tulikaa kama familia na Sikukuu ya Pasaka ndiyo Ray na Kanumba walikuwa wapeane mikono na kumaliza tofauti zao lakini Mungu akamchukua kabla ya siku hiyo kufika,” alisema Mama Kanumba.
Marehemu Steven Kanumba enzi za uhai wake.
Alipotafutwa Steve Nyerere kuhusiana kuhusishwa katika ugomvi wa Ray na Kanumba, alifunguka:

“Mama anatapatapa, Ray mtu mzima mimi nitamgombanisha na Kanumba kwa lipi? Siyo kweli. Mbona mimi sikuwa na tatizo lolote kati yao, Kanumba hadi anafariki tulikuwa vizuri, kabla  hajafa alinipigia simu twende Mashujaa (bendi). Ningekuwa mimi ni tatizo tungeelewana? Halafu kwanza kwa nini hayo maneno yaibuke sasa? Nashindwa kumuelewa huyo mama.” 

0 comments: