AIBU:HAKUNA UBISHI SITTI MTEMVU KADANGANYA UMRI

LILE sakata la Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zubeir Mtemvu kudaiwa kudanganya limeingia ukurasa mwingine kufuatia ufukunyuku wa gazeti hili kubaini kuwa, miaka 25 ndiyo sahihi kwake.
Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zubeir Mtemvu.
Kufuatia ushindi alioupata siku ya shindano la kumsaka Miss Tanzania 2014 lililofanyika Oktoba 11, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Mlimani City, kuliibuka madai kwamba mrembo huyo alidanganya umri.
MADAI YA JUKWAANI
Awali, akiwa jukwaani kujitambulisha na kujibu maswali, mlimbwende huyo alishika kipaza sauti na kusema:
“My name is Sitti Mtemvu,  ‘am  eighteen years old (jina langu ni Sitti Mtemvu, nina miaka kumi na nane).
Hapo ndipo palipoanzia utata, wanaomjua Sitti walianika umri wake kwamba, ana miaka 25 huku wakianika tarehe ya kuzaliwa kwake kwamba ni Mei 31, 1089. Miandao ikaanza kumponda kwamba alidanganya umri hivyo halimfai tena!
LUNDENGA ATOA TAMKO, ATETEA
Kufuatia hali ya hewa kuchafuka kwenye mitandao, redio na magazeti akishutumiwa Sitti, Oktoba 21, mwaka huu, mratibu wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga aliitisha mkutano na vyombo vya habari.
Ads by TheFreeHD-Sports TV 1.1Ad Options
Cheti cha kuzaliwa cha Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu.
Katika mkutano huo ambao Sitti naye alishiriki sanjari na mama yake mzazi, Lundenga alisema vyeti vya kuzaliwa alivyowasilisha mshiriki huyo kama washiriki wengine, vilionesha ana miaka 23, alizaliwa 1991, Temeke jijini Dar.

UTATA WAIBUKA
Utata ulianza kuibukia hapo kwenye maneno ya kutoka kwenye kinywa cha Lundenga kwani alisema cheti hicho kilitolewa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Uzamini (Rita) Septemba, mwaka huu ikiwa ni siku 32 tu kabla ya shindano la Mlimani City.

MASWALI
Waandishi walitaka kujua hivi; kama cheti hicho kilitolewa Septemba 9, mwaka huu na Sitti amesoma Marekani ambako mtu huwezi kwenda mpaka uwe na paspoti na ili upate paspoti lazima uwe na cheti cha kuzaliwa je, yeye alitumia cheti gani? Maana alikwenda Marekani kati ya mwaka 2010 na 2011.
Leseni ya udereva ya miss Tanzania Siti Mtemvu.
Sitti alilijibu swali hilo kuwa, cheti hicho kilipotea lakini akashindwa kukitaja kituo chochote cha polisi alichopeleka madai ya kupotelewa kwa cheti na kuishia kusema
vyombo vya habari vinamfuatafuata sana.
Ads by TheFreeHD-Sports TV 1.1Ad Options
UFUKUNYUKU WAANZA
Kufuatia mlolongo huo wote, ndipo timu ya uchunguzi ya Magazeti Pendwa ya Global Publishers ikaingia mtaani na kuanza kuchimba ukweli wa umri wa binti huyo.
Katika chanzo cha uhakika kutoka katika idara husika ya kutoa paspoti, faili la Sitti lilisomeka hivi: (tunaandika kwa Kiswahili tu).
Jina la ukoo: Mtemvu.
Jina: Sitti Abbas.
Utaifa: Mtanzania.
Tarehe ya kuzaliwa: May 31 1989.
Tarehe ya kutolewa: 17 Feb 2007.
Tarehe ya Mwisho wa matumizi: 14 Feb 2017.
Pasipoti ya miss Tanzania Siti Mtemvu.
Ads by TheFreeHD-Sports TV 1.1Ad Options
SHULE ALIYOSOMA UGANDA
Ufukunyuku wa gazeti hili ulikwenda mbele zaidi hadi kwenye Shule ya Sekondari ya Hana Mixed iliyopo Mji wa Nsangi, Kampala, Uganda ambako Sitti alisoma kidato cha tano na sita.
Akizungumza na gazeti hili kwa sharti la jina lake kutoandikwa gazetini, mwanafunzi mmoja alisema kuwa, mwaka 2006 Sitti aliingia shuleni hapo kidato cha tano akiwa na miaka 17. (Piga hesabu mpaka mwaka huu).
BETHIDEI YAKE 2007
Mwanafunzi huyo akazidi kudai kuwa, Mei 31, 2007, Sitti akiwa kidato cha sita, alifanya sherehe fupi ya kuadhimisha kuzaliwa kwake ‘bethidei’ ambapo alisema anatimiza mwaka wa 18.
Sitti Abbas Zubeir Mtemvu.
Katika kasherehe hako ambako hakakuwa rasmi, waliohudhuria ni kijana mmoja na wanafunzi waliokuwa wakilala chumba kimoja na Sitti. Sitti alimaliza kidato cha sita Novemba 2007.
MNYAMBULISHO WAKE
Kwa hesabu za haraka, Sitti alianza darasa la kwanza akiwa na miaka 6 (1995). Darasa la 7 akamaliza akiwa na miaka 12 (2001). Alianza kidato cha kwanza akiwa na miaka 13 (2002), akamaliza kidato cha 4 akiwa na miaka 16 (2005). Akiwa na miaka 17 alianza kidato cha 5 (2006), akamaliza cha 6 akiwa na miaka 18 (2007).
Kwa mahesabu hayo, mlimbwende huyo alizaliwa mwaka 1989 sawa na hati yake ya kusafiria na leseni ya udereva ambavyo vyote vinaonesha kuwa alizaliwa mwaka huo. Hii ni aibu kwa Lundenga!

0 comments: