DIDA AMTANGAZA MUME WAKE MPYA ,BAADA YA KUACHANA NA MUME WAKE WA ZAMANI
SIKU chache baada ya kudai hawezi kuolewa kwa sasa, mtangazaji wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kupitia Radio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’, ameonesha matumaini mapya ya kuolewa baada ya kumwanika mchumba’ke mpya.
Dalili za matumaini hayo mapya
zilionekana usiku wa kuamkia Alhamisi iliyopita katika sherehe yake ya
kuzaliwa (bethidei) iliyofanyaka nyumbani kwake, Mwananyamala jijini Dar
na kuhudhuriwa na mastaa kibao Bongo.
Miongoni mwa wasanii waliohudhuria hafla
hiyo ya kufuru ni pamoja na malkia wa Mipasho Bongo, Khadija Kopa na
waigizaji; Chuchu Hans, Jacob Steven ‘JB’, Rose Ndauka, Salma Salmin
‘Sandra’, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, Jeniffer Kyaka ‘Odama’,
Maimatha Jese na wengine kibao ambao walimpa Dida kampani ya nguvu na
kumtunza fedha na zawadi mbalimbali.
Kama hiyo haitoshi, kwenye hafla hiyo,
kulitawaliwa na vinywaji vya kila aina huku kukiwa akichinja mbuzi
watatu maalum kwa ajili ya sherehe hiyo sambamba na kuku kibao wa
kienyeji, nyama za kila aina, msosi wa nguvu na pombe za kumwaga.
Wakati sherehe ikiendelea, Dida aliibua
minong’ono ya aina yake baada ya kutambulisha uwepo wa shemeji zake
waliotoka Arusha ambao walimwakilisha mchumba wake katika pati hiyo.
“Jamani humu ndani kuna watu mbalimbali ambao wamefika kuniunga mkono, mkiwemo wasanii wanahabari pamoja na watangazaji wenzangu, lakini kikubwa zaidi napenda kutambua uwepo wa shemeji zangu waliofunga safari kutoka Arusha, wamekuja kuniunga mkono, nimefurahi sana,” alisikika Dida.
“Jamani humu ndani kuna watu mbalimbali ambao wamefika kuniunga mkono, mkiwemo wasanii wanahabari pamoja na watangazaji wenzangu, lakini kikubwa zaidi napenda kutambua uwepo wa shemeji zangu waliofunga safari kutoka Arusha, wamekuja kuniunga mkono, nimefurahi sana,” alisikika Dida.
Ulipofika muda wa kutoa zawadi, mmoja wa
mashemeji zake hao aliyejitambulisha kwa jina la Feisal alishika kipaza
sauti na kusema alitinga kwenye hafla hiyo kumwakilisha ndugu yake
(jina alilihifadhi) ambaye alimtuma amwambie Dida kuwa amemzawadia gari
lenye thamani ya Sh. milioni 26 za madafu ambalo siku si nyingi litatua
Dar.
“Hehee my new baby, huyo ndiye my new baby jamani na hawa ndiyo mashemeji zangu wa ukweli,” alipaza sauti Dida.
Alipoulizwa na mwandishi wetu juu ya mipango yake na mchumba huyo mpya, Dida alifunguka:
“Huyo ndiye mwanaume wangu wa sasa muda ukiwadia nitaanika kila kitu, bado mapema mno kuzungumza mengi,” alisema Dida ambaye kama ataolewa na mwanaume huyo itakuwa ndoa ya nne.
Dida aliyemwagana na Ezden Jumanne miezi
kadhaa iliyopita, kabla ya hapo aliwahi kuolewa na wanaume wawili
tofauti ambao alimwagana nao kwa talaka.
0 comments: