UNAAMBIWA DIAMOND KUFUNGWA JELA MIAKA MITATU! HABARI KAMILI SOMA HAPA
Kufuatia tukio la staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
kuonekana jukwaani na sare zinazoaminika kuwa za Jeshi la Wananchi
(JWTZ) kisha kukamatwa kwa kundi lake la Wasafi Classic Baby (WCB) na
meneja wake, Babu Tale, kuna uwezekano wa jamaa huyo kufungwa jela miaka
miwili au mitatu.
Kwa mujibu wa chanzo chetu ndani ya jeshi
la polisi, baada ya jeshi kutoa tamko kuwa ni kinyume cha sheria, juzi
Diamond alitakiwa kwenda kujisalimisha polisi lakini hakufanya hivyo
jambo lililosababisha wenzake kukamatwa na kuwekwa nyuma ya nondo za
mahabusu ya Oysterbay, Kinondoni jijini Dar.
Ilisemekana kwamba baada ya Wasafi (madensa wa Diamond) kukamatwa, Babu Tale naye alifikishwa katika kituo hicho ambapo maafisa kadhaa wa jeshi la polisi walionekana katika eneo hilo wakiweka ulinzi mkali.
Ilisemekana kwamba baada ya Wasafi (madensa wa Diamond) kukamatwa, Babu Tale naye alifikishwa katika kituo hicho ambapo maafisa kadhaa wa jeshi la polisi walionekana katika eneo hilo wakiweka ulinzi mkali.
Madensa wa ‘Diamond Platnumz’ wa kundi la Wasafi Classic Baby (WCB) wakisindikiza shoo yake.
Chanzo hicho kilieleza kwamba, siku ya
tukio Oktoba 21, mwaka huu, uongozi wa Diamond ulipewa muda wa kujieleza
kabla ya saa 2:00 asubuhi lakini haukufanya hivyo ndipo hatua hiyo
ikachukuliwa.
Hata hivyo, baadhi ya watu walikuwa wakihoji kwa nini jeshi la polisi lilimshikilia Babu Tale peke yake bila Diamond lakini vyanzo vilieleza kuwa mwanamuziki huyo huenda alikuwa safarini.
Hata hivyo, baadhi ya watu walikuwa wakihoji kwa nini jeshi la polisi lilimshikilia Babu Tale peke yake bila Diamond lakini vyanzo vilieleza kuwa mwanamuziki huyo huenda alikuwa safarini.
Diamond akiendelea kutoa burudani jukwaani.
Ilielezwa kwamba wanaomsaka Diamond na waliowakamata Wasafi ni
wanajeshi wa Military Police (MP) ambao waliwabwaga jamaa hao kituoni
hapo kisha kuendelea na mambo yao. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Dar, Camillus Wambura alisema bado hajawasiliana na kituo cha Oysterbay kuhusu suala hilo na hajapata taarifa kwa kuwa kesi hiyo inachunguzwa na iko chini ya Mkuu wa upelelezi wa Mkoa.
Akijibu kuhusu taarifa za uongozi wa Diamond na Diamond kupewa muda wa kujieleza, Kamanda Wambura alijibu:
Diamond Chege wakifanya yao.
“Uchunguzi unafanywa huko (Oysterbay). Kwa sasa hivi sina taarifa
hiyo nina mambo mengi sana. Kwa hiyo kwa sasa hivi uchunguzi unafanywa
chini ya Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa. Sijapata nafasi ya kujua wamefikia
wapi katika uchunguzi wa suala hilo.”Mapema wiki hii, Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) lilitoa taarifa kwa vyombo vya habari likipiga marufuku raia kuvaa sare za jeshi.
Kwa mujibu wa mwanajeshi wa JWTZ ambaye aliomba hifadhi ya jina kwa kuwa si msemaji wa jeshi hilo, taaluma yake ya sheria imemfanya kuchimba kwa undani suala hilo na kugundua kuwa endapo Diamond atapatikana na hatia atapigwa faini au kwenda jela miaka miwili au mitatu au vyote, yaani faini na kifungo.
Alisema kosa la Diamond ni kushindwa kutii
wito kwani alitakiwa kuripoti mwenyewe polisi hivyo lazima atapanda
mahakamani kujibu shitaka hilo na lile lenyewe la kutumia sare za jeshi
hilo.Chanzo hicho kilidai kwamba si mara ya kwanza kwa jamaa huyo
kuingia kwenye kashikashi kama hiyo kwani kuna kipindi alikwenda Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambapo alionekana na sare hizo stejini
na akapewa onyo lakini safari hii amejiongeza tena kuonesha kuwa ni
kichwa ngumu.
0 comments: