''MPENZI WANGU ANANISALITI KWA WANAWAKE WEMBAMBA,SASA SIJUI MIMI ALINITAKA WA NINI?

MIMI ni msichana mwenye umri wa miaka 23
naitwa Samantha wengi hunitania na kuniita
Bonge, elimu yangu sio mbaya sana na nimtoto
wa familia yenye maisha mazuri kias fulani,
Nimekuwa nikiteswa na mfumo wa mapenzi yetu
mimi na mpenzi wangu maana nashangaa tangu
tuanze mahusiano nimemfumania zaidi ya mara 4
na
mimi bado nampenda jamani kibaya zaidi
wanawake wote naomnasa nao ni wembamba
kama njiti, Sasa sielewi kama alikuwa anapenda
wanawake wembamba kwanini anitongoze? Alafu
ukizingatia huyo mpenzi wangu ni mwembamba
mrefu inamaana haoni kama tunaendana?..
Na mimi natongozwa sana na mkaka mmoja hivi
tupo nae kazini kwangu nafanya nae kazi ofisi
moja yeye ni mesenja Sijui nimkubalie ili ngoma
iwe droo? Naombeni ushauri jamani maana Admin
amaniambia niwaombe nyinyi ushauri yeye hana
la kusema.


0 comments: