MTOTO WA NAIBU WAZIRI WA ZAMANI WA AFYA JONAS NKYA AKANA TUHUMA ZA KURUSHIANA RISASI NA MAMA YAKE
Jonas
Nkya mtoto wa Naibu Waziri wa zamani wa Afya na Mbunge wa Morogoro
kusini masgariki Lucy Nkya amewaambia waandishi wa habari kwamba habari
zilizozagaa kwenye mitandao ya kijami kwamba amerushiana risasi za moto
na mama yake mzazi ofisini kwao leo mkoani Morogoro.
Jonas
Nkya amesema kilichotokea alipokwenda ofisini hapo kuchukua gari
alielekee shamba bastola ilidondoka chini na ikajifyatua risasi moja na
kuzua taharuki kwa watu. Kwanza mimi sina ugomvi wowote na mama yangu
mimi nilikua shamba narudi nashangaa nimezungukwa na waandishi wa habari
wakitaka kujua ukweli wa habari hizi.
Mimi nashanga habari zilizozagaa kwenye mitandao zimetokea wapi.
0 comments: