MTU MZIMA HOVYO...ANASWA AKIMTEKA MTOTO WA SHULE,AANGUSHIWA KICHAPO KITAKATIFU
HALI
bado tete! Polisi wa Kituo cha Magomeni jijini Dar, wamemkamata baba
mmoja
aliyetambuliwa kwa jina moja la Omar baada ya kupokea kipigo ‘hevi’ kutoka kwa raia wenye hasira kali akihusishwa na utekaji wa denti wa Shule ya Msingi Mwalimu Nyerere iliyopo maeneo hayo.
aliyetambuliwa kwa jina moja la Omar baada ya kupokea kipigo ‘hevi’ kutoka kwa raia wenye hasira kali akihusishwa na utekaji wa denti wa Shule ya Msingi Mwalimu Nyerere iliyopo maeneo hayo.
Denti
wa Shule ya Msingi Mwalimu Nyerere, Magomeni (mwenye sare za shule)
aliyenusurika kutekwa na njemba inayotambuliwa kwa jina moja la Omar.
Tukio hilo lililokusanya kadamnasi lilijiri wikiendi iliyopita,
Magomeni-Kagera, Dar wakati mwanafunzi huyo akitokea shuleni.Kwa mujibu
wa mashuhuda, denti huyo alipofika eneo hilo, baba huyo alimsalimia na
baada ya kujibiwa salamu yake alianza kumchombeza kwa maneno
matamu-tamu.
Baadhi ya raia wenye hasira kali waliotoa kipigo ‘hevi’ kwa Bw. Omar wakiwa wametanda eneo la tukio.
Akizungumza na Uwazi lililofika eneo la
tukio ndani ya ‘dakika sifuri’, denti huyo aitwaye Laila alisema licha
ya kuitikia salamu ya jibaba huyo na kumuamkia bado aliendelea
kumchombeza na kila alipojaribu kumkwepa ilishindikana.Makamanda wa Polisi waliofika eneo la tukio kumuokoa mtuhumiwa.
Njemba huyo alivuka mipaka na kumshika mkono na kutaka kumvutia ndani
ya gari lililokuwa karibu yake ndipo Laila alipoamua kupiga mayowe ya
kuomba msaada na hatimaye kuokolewa na wasamaria wema waliokuwa wakipita
njia.”
Mwanafunzi huyo aliendelea kusema:
“Alianza kunifuatilia tangu kule, akanisalimia hujambo nikamjibu
sijambo, akaniambia tena kwenu hawajambo, nikamjibu hawajambo,
akaendelea kuniambia eti, nimfuate akanipe lambalamba, mimi nikakataa
kwa sababu mama alinikataza kukubali kupewa lifti na vitu vingine kutoka
kwa watu nisiowajua tangu aliposikia habari za watoto kutekwa na Noah
nyeusi.Wasamaria wema wakimuokoa mtoto huyo.
“Kila kitu nilimkatalia lakini yeye akawa anaendelea kuniambia maneno
yake na kuanza kunivuta ndipo nikaona sasa naenda kufa hivyo ikanibidi
nipige kelele ndiyo watu wakatokea na kumkamata kisha kuanza kumpiga
mpaka walipofika polisi.”
Gazeti hili lilizungumza na mtuhumiwa
aliyekuwa amehifadhiwa ndani ya gari, alipoulizwa kuhusiana na tuhuma
hizo alimuomba paparazi wetu kabla ya yote kwanza amuokoe na kifo kutoka
kwa wananchi wenye hasira kali.Binti akiwa kwenye gari mara baada ya kuokolewa.
“Chondechonde ndugu yangu, naomba kwanza mnilindie usalama wangu, hao
jamaa wanataka kuniua bila sababu, mimi wala sikuwa na nia mbaya na
huyo binti wananizushia tu, nilikuwa namsalimia tu,” alisema Omar
kupitia upenyo mdogo wa juu ya dirisha la gari alilohifadhiwa.
0 comments: