Ni wasanii gani wa bongo walimshtua Davido kwa shangwe kwenye Fiesta Dsm?
Unaambiwa weekend iliyopita kwenye Fiesta ya Dar es salaam mwimbaji Davido wa
Nigeria alitumia dakika zake zote kutazama screen zilizokua zimewekwa
nyuma ya stage ya Fiesta baada ya kusikia shangwe zilizokua zinapigwa
baada ya Wakali wengine
kupewa time ya kumiliki stage.
Alilazimika kutazama TV hizo kwa umakini baada ya kuona shangwe walilopata WEUSIambapo
mashabiki walikua wanaimba nyimbo zao kwa muda mrefu ambapo Davido
kabla ya kuuliza alitumia muda mrefu kuwatazama kwa makini baada ya
kushangazwa na shangwe walilokua wanapata WEUSI hawa.
Baada
ya Wakali hawa kumaliza show Davido alianza kuuliza ni kina nani na
wana umaarufu kiasi gani ambapo mmoja wa marafiki zake amesema stori
hazikuishia uwanjani kwenye Fiesta bali mpaka Hotelini Davido alionyesha
kushangazwa na shangwe la WEUSI na kuwaongelea tena.
Hii itafanya idadi ya Wasanii wa bongo wanaofahamika na Davido iongezeke
manake alipokuja juzi Tanzania alihojiwa muda mfupi tu baada ya kutua
kwenye uwanja wa ndege na kusema msanii pekee wa Tanzania anaemfahamu
ni Diamond Platnumz.
Mengine aliyoyasema ni kwamba kwenye album yake mpya inayotoka mwanzoni
mwa 2015 wameshirikishwa wasanii wachache kutoka Afrika ambao ni pamoja
na Diamond na Mafikizolo na kwamba kuna wasanii wawili wakubwa wa
kimataifa aliowashirikisha ambao hatowataja kwa sasa.
0 comments: