Unafahamu ‘kibarua kipya’ alichopewa Chris Brown na Mahakama? Soma hapa mtu wangu. Chris_brown_court_AP
Stori
mpya ninayokuletea mtu wangu wa nguvu inamhusu mwanamuziki Chris Brown,
huenda
hujapata nafasi ya kukutana na stori zake hivi karibuni,
nakuletea hii ambayo ni latest zaidi kuhusiana na jamaa huyo.
Ripoti ya nguvu niliyoipata TMZ kuhusiana
na Chris Brown inasema jamaa kapewa dili la nguvu na mahakama
litakayomuweka busy mpaka Januari Mwaka 2015, kutokana na kibarua
chenyewe kuwa na ratiba tight ya aina yake.
Chris Brown amepewa ‘dili’ la kufanya kazi za kijamii kwa masaa nane
kila siku, na kwa mujibu wa ratiba aliyopewa na mahakama anatakiwa
afanye kazi hizo kwa siku 4 kila wiki, ikimaanisha ni siku 1 tu ndani ya
wiki kuanzia Jumatatu mpaka Ijumaa ambazo ‘atadeal’ na mambo yake
mengine.
Utetezi wa daktari wake huenda usimuokoe Chris kwenye ‘kitanzi cha
ajira’ hiyo kutokana na matukio kadha aliyoyafanya kipindi akiwa chini
ya uangalizi wa mahakama juu ya mwenendo wake baada ya kukabiliwa na
kesi ya kumtwanga makonde mpenzi wake wa zamani, Rihanna.
0 comments: