CATHY WA BONGO MUVI,AMUA KUBADILI JINA KISA LINA MKOSI
MKONGWE wa
filamu kitambo, Sabrina Rupia ‘Cathy’ amesema kuwa jina analotumia
katika sanaa lina mkosi hivyo yuko kwenye mkakati wa kulibadilisha na
kujipa jina lingine labda linaweza kumkaa vizuri.
Akizungumza na mwandishi wetu, Cathy
alisema anaona jina hilo lina mkosi kwa sababu linazungumzwa vibaya na
baadhi ya wasanii wenzake hata kama kuna kitu ambacho hakijui ni lazima
lihusishwe jina lake kitu ambacho anakiona kama jina hilo lina nuksi.
“Unajua naona jina hili lina mkosi kwa
sababu kitu kifanyika labda mimi nimepita tu basi litatajwa jina langu
kitu ambacho mimi sikipendi na kuona labda lina matatizo jamani, haliko
sawa kuendelea kuwa nalo,” alisema Cathy huku akidai yuko katika
mikakati ya kutafuta jina lingine zuri ambalo anaona linamfaa. zaidi.
0 comments: