Utata watawala msiba wa nahodha wa Bafana Bafana, Senzo Meyiwa
Utata mkubwa umeukumba msiba wa aliyekuwa nahodha na mlinda mlango wa Bafana Bafana, Senzo Meyiwa aliyeuwa kwa kupigwa risasi nyumbani kwa mpenzi wake, Kelly Khumalo, Jumapili iliyopita.
Katika tukio hilo, watu hao walichukua simu peke yake na Meyiwa aliyekuwa pia akiidakia timu ya Orlando Pirates alifariki akipelekwa hospitali baada ya kupigwa risasi na watu hao.
Familia ya Meyiwa imesema haitaki kumuona Khumalo msibani na kama akienda watamfukuza.
Katika mji wa uMlazi, Mandisa Mkhize ambaye ni mke wa Meyiwa amekosolewa kwa kutokuombeleza kama mila za kabila lao zinavyomtaka. Majirani wanadai kuwa Mandisa amekataa kuomboleza kimila kwakuwa alikuwa na hasira kuwa mume wake Meyiwa alimuacha kwenye party na kwenda kupata dinner nyumbani kwa Khumalo.
“Alimuabisha sana. Hata ule ukweli kwamba alikufa akionesha upendo kwa Khumalo kumemuabisha sana mke wake,” alisema jirani yake.
0 comments: