ASKOFU GEOR DAVIE AVUNJA NDOA YA SEKRETARI WAKE
KIMENUKA! Ndoa
iliyodumu kwa miaka 15 kati ya Wiston Lotta (52) na Pamella Geofrey
(40) imevunjwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kufuatia ushahidi
mzito uliotolewa mahakamani hapo kumridhisha Hakimu Hawa Mghuruta.
Askofu Mkuu wa Huduma na Ngurumo ya
Upako, George David ‘Geor Davie’ yenye makao makuu yake jijini Arusha
ndiye aliyetajwa na mahakama hiyo kuwa ni chanzo cha kuvunjika kwa ndoa
hiyo ya Pamella ambaye alikuwa ni sekretari wa kiongozi huyo wa dini
baada ya ujumbe mfupi wa maneno (SMS) ukionesha mapenzi kunaswa kwenye
simu ya mwanamke huyo ukitokea kwa Geor Davie.
Ushahidi uliotolewa na mwanaume ulidai
kuwa mgogoro wa ndoa yake ulitokana na mkewe kuwa na uhusiano wa
kimapenzi na Askofu Geor Davie.
Akisoma hukumu ya kesi hiyo Namba 01 ya
mwaka 2012, Hakimu Mghuruta alisema kabla ya hukumu, mahakama
ilizingatia ushahidi wa mashahidi watano wa upande wa mlalamikaji.Mke wa mtu Pamella Geofrey (katikati) anayedaiwa kutoka kimapenzi na boss wake, Askofu George David ‘Geor Davie’.
Alimtaja mtoto wa kwanza wa wanandoa
hao, Sifael Wiston (15) kwamba naye aliieleza mahakama hiyo namna mama
yake alivyokuwa akizini nje ya ndoa kwa kukutana na Geor Davie ndani ya
gari lake lenye rangi ya silva wakati wa usiku baba yake akiwa safarini.
Mtoto huyo alianika kwamba, walikuwa
wakipelekewa juisi na bajia ndani ya gari hilo lenye pazia kisha wao
kufunga vioo kwa muda mrefu huku likionekana kutikisika, ushahidi ambao
uliwashangaza waumini wa kanisa la askofu huyo.
Askofu George David ‘Geor Davie’ akitoa huduma ya maombezi kwa waumini.
Wiston ambaye alikuwa msaidizi wa Geor
Davie, alifungua kesi ya kudai talaka kwa Pamella ili kufikia ukomo wa
shauri hilo ambalo lilianza kusikilizwa na Baraza la Usuluhishi wa Ndoa
mwaka 2007 lakini ilishindikana kwa vile mkewe alipeleka sababu za uongo
kuwa alikuwa akinyanyaswa hivyo kuikimbia nyumba.
Hakimu Mghuruta ameamuru mali zote
yakiwemo magari matatu, nyumba iliyopo Sakina na vitu vingine zibaki
chini ya mlalamikaji lakini Pamella anaruhusiwa kwenda kuwasalimia
watoto wake. Hata hivyo, mahakama ilimtaka Pamella kutowarubuni watoto
hao kiasi cha kuathiri masomo yao.
0 comments: