BAADA YA WEMA SEPETU KUMMWAGA DIAMOND...MAMA WEMA AFANYA BONGE LA SHAREHE



Supastaa ‘grade one’ wa sinema za Bongo, Wema Sepetu ‘madam’ akipozi.

CHEREKO chereko! Siku chache baada ya supastaa ‘grade one’ wa sinema za Bongo, Wema Sepetu ‘madam’ kummwaga King of Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, mama mzazi wa mwigizaji huyo, Mariam Sepetu ameangusha sherehe ya nguvu kama ishara ya kuonesha ‘amekunwa’ na tukio hilo, Ijumaa Wikienda linashuka nayo mstari kwa mstari.

 

 

TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, kutokana na mama huyo kutobariki uchumba wa mwanaye na Diamond ambaye pia anajulikana kwa jina la Dangote kwa muda mrefu, habari za uchumba huo kuvunjika zilipochapishwa kwenye Gazeti la Ijumaa ‘Kubwa’ toleo lililopita, moyo wake ulijawa na furaha.

“Mama Wema alichukizwa kwa kiasi kikubwa na mapenzi ya wawili hao kutokana na kile alichoamini kuwa, Diamond hakuwa na mapenzi ya dhati kwa mwanaye zaidi ya kutegemea nyota yake impe mafanikio ndiyo maana akafanya pati hiyo fupi nyumbani kwake Sinza-Mori, Dar,” kilisema chanzo hicho.
Wema Sepetu ‘madam’ akifurahi na mama yake, Mariam Sepetu
SHEREHE ILIVYOKUWA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga unga kwamba, sherehe hiyo ilikuwa ni ya aina yake kwani mama Wema aliwaita mashosti zake, wakaandaa ‘menu’ ya ukweli kabisa, wakasherehekea lakini bahati mbaya Wema hakuhudhuria.


SOMA HIZI 

 

“Wema hakuweza kuhudhuria sherehe hiyo kutokana na kubanwa na majukumu mengine. Bi mkubwa aliwaita marafiki zake, wakafungua shampeni, wakala, wakanywa na kucheza muziki kufurahia Dangote kupigwa chini,” kilisema chanzo hicho.
Dangote wakati akiwa na Penniel Mungilwa ‘Penny’
MAMA NA CHUKI YA MUDA MREFU
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu motomoto kuwa, mama Wema alipiga cherekochereko za kutosha siku hiyo kwani alikuwa akimchukia Diamond kwa muda mrefu.


 
“Mama Wema chuki zake kwa Diamond hazitaisha kamwe kwa kuwa hampendi tu kutokana na kuona mwanaye hasongi mbele kimaendeleo kama alivyo Diamond ambaye akiachana na Wema mambo yake hayamwendei vizuri kama anavyokuwa na mwanaye.”

Diamond wakati akiwa na Jokate Mwegelo.
MAMA WEMA ANENA
Baada ya wanahabari wetu kunasa maelezo hayo ya chanzo, walimvutia waya mama Wema ambaye alikiri kufanya sherehe fupi baada ya mwanaye kummwaga Diamond.
“Mimi naona huu ndiyo mwisho wa Wema na Diamond na siku zote nasema hakuna uhusiano ukadumu bila baraka za wazazi, niseme tu, sitaki kumuona ndugu yeyote wa Diamond kwangu, kama mahari wakatoe kwa Penny siyo kwa mwanangu,” alisema mama Wema.

Wema Sepetu,'Madam' akiwa na Diamond Platinumz.
TUJIKUMBUSHE
Kumwagana kwa Wema na Diamond safari hii, ni mara ya nne. Awali walimwagana, wakarudiana, wakamwagana tena, Diamond akatua kwa Jokate Mwegelo, wakarudiana tena na Wema, wakaja mwagana tena, Diamond akatambaa na Penniel Mungilwa ‘Penny’, wakamwagana, karudiana na Wema, sasa  wamemwagana tena.

0 comments: