HATIMAYE YULE MTOTO WA MAAJABU "MTOTO WA NDEGE" AOKOKA

MTOTO Happiness Lyoba (10) ambaye aliripotiwa kuwa mwingi wa vituko vya maajabu, ikiwamo kuonekana akishuka katika ndege huko Zanzibar, ameripotiwa kuokoka katika Kijiji cha Mkokozi, wilayani Mkuranga, Pwani.
Mtoto Happiness Lyoba (10) akisoma Biblia.
Akizungumza na gazeti hili, mama wa mtoto huyo, Salah Zefania alisema mwanaye huyo alitoroka tena Septemba 16, mwaka huu na kukamatiwa eneo la Feri jijini Dar es Salaam, akidai kuwa ameitwa  na baba yake.
Baada ya kumkamata na kuanza kurejea naye kijijini Mkokozi ambako amehifadhiwa na msamaria mwema, alisema alipata simu nyingi za watu kumpa pole kwa tukio hilo, hali iliyomshangaza kwani hakuelewa watu hao walipataje habari hizo.
Mama mzazi wa mtoto Happiness Lyoba , Salah Zefania.
Miongoni mwa simu hizo ni pamoja na ya Mwinjilisti wa kanisa lao la Kisabato Mbagala aliyemtaja kwa jina la Jacob Mayala ambaye alihitaji kumuombea mtoto wake. ‘’Ni kweli Mwinjilisti huyo alifika Mkokozi na kufanya maombi maalumu yaliyoambatana na kufunga kwa siku kadhaa. Hali ya mwanangu kwa sasa ninakubaliana nayo maana amegeuka kuwa  binadamu ambaye  nilimtarajia, Happiness  hakuwa hivi maana alizidisha vituko vya maajabu,” alisema.
Mtoto Happiness Lyoba akiwa na mama yake.
Mama huyo amewaomba Watanzania wamsaidie mwanaye kusoma kwani hivi sasa anajitambua tofauti na huko nyuma.“Mimi kipato changu ni kidogo na huku niliko ni mbali sana, hakuna shule karibu, kazi yangu ni kilimo cha mbogamboga na tena hapa ninapoishi nimehifadhiwa tu, ninaomba msaada ili mtoto wangu aende shule,” alisema mama huyo akidai kuwa Ustawi wa Jamii ulimshauri kumweka binti yake mbali na maeneo aliyokuwa akiishi.
“Nilishauriwa asirudi  Kitunda kwa muda huu maana huko ndiko alikoanza kupatwa na hali ambayo naamini ilikuwa ni mapepo,” alisema.
Mtoto na mama wakisali pamoja.
HAPPINES  LYOBA

Kwa upande wake, Happines alisema anahitaji kusoma na kwamba matukio aliyokuwa akiyafanya hakujua yalivyotokea.
Mtu yeyote aliyeguswa na hali ya mtoto huyu ambaye akili yake imerejea kuwa ya kawaida kufuatia maombi ya kila siku, anaweza kuwasiliana na mama yake kwa namba 0768 632693. 

0 comments: