HUZUNI!! MWALIMU AMUA MWANAFUNZI KWA KUMCHAPA VIBOKO
Mwanafunzi
wa darasa la tano katika Shule ya msingi ya Kiuu Kenya amefariki dunia
baada ya kupigwa na mwalimu wake kwa kufeli somo lake la Kiswahili.
Familia ya mtoto huyo Joseph Waburi mwenye umri wa miaka kumi imesema mtoto huyo alikuwa na nidhamu ya hali ya juu.
Mama
wa mwanafunzi huyo Grace Muthoni amesema mtoto wake alienda shule
Jumatatu asubuhi na aliporudi alianza kulalamika maumivu ya kichwa na
shingo, siku iliyofuatia alimpeleka Zahanati ya Wilaya ya Nyagiti level
4.
Siku
ya pili alilazimika kumrudisha Hospitali baada ya hali yake kuzidi kuwa
mbaya, daktari akashauri ahamishiwe katika Zahanati ya Muran’ga Level 4
kwa matibabu zaidi.Wakati akisubiri gari la wagonjwa akafariki dunia.
Mama
huyo amesema uchunguzi wa awali unaonyesha mtoto wake alipigwa na
Mwalimu na kupata majeraha kichwani na shingoni, mwili wake umehifadhiwa
kwa ajili ya uchunguzi kubaini sababu za kifo chake.
Mwalimu
anayedaiwa kumpiga Mwanafunzi huyo alikimbia kujificha shimoni baada ya
kusikia taarifa za kifo, huku Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Joseph Mwenda
akikanusha uvumi kwamba mtoto huyo alifia shuleni
0 comments: