JAJI WARIOBA, NISINGEVUNJWA MOYO NA ‘MAMLUKI’ WA KISIASA
Jaji
Joseph Sindwe Warioba akitolewa nje ya ukumbi wa Ubungo Plaza jijini
dar kwenye mdaharo wa kujadili umhimu wa wananchi kuitambua rasimu ya
katiba, mdaharo uliokuwa umeandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere chini
ya Mwenyekiti wake Joseph Butiku.
Kwako Jaji Joseph Sinde Warioba.Nakupa
pole kwa misukosuko ya hapa na pale inayokupata, tangu ulipokabidhiwa na
Rais jakaya Kikwete jukumu la kuongoza Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Najua kwa sababu za usalama wako
binafsi, itakuwa vigumu kwa mimi na wewe kukutana ili nikufikishie
ujumbe wangu kwako. Kwa kuzingatia hilo, ngoja nikufikishie ujumbe
kupitia safu hii.Mimi sikuzaliwa Septemba 3, 1940, Bunda mkoani Mara
kama wewe. Nakuhakikishia kuwa sikusomea kwenye Chuo Kikuu cha Afrika
Mashariki na kuhitimu mwaka 1966. Sijawahi kuwa mwanasheria mkuu wa nchi
hii kuanzia mwaka 1966 hadi 1968 kama wewe na sijawahi kuwa Waziri Mkuu
na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania kama wewe tangu mwaka 1985 hadi
1990, wala sina ndoto hizo.
Sijawahi kuwa waziri mkuu na makamu wa
rais wa nchi hii kwa sababu sina sifa hata moja inayoweza kufanya
nikashika wadhifa huo mkubwa katika nchi kama wewe. Sijawahi kuwa jaji
katika Mahakama ya Sheria ya Afrika Mashariki wala sijawahi kuwa waziri
wa sheria wa nchi hii.
Sikuteuliwa na Rais Benjamin Mkapa kuongoza tume maalum ya kupambana na rushwa kama wewe wala sijawahi kuwa mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama wewe.
Sikuteuliwa na Rais Benjamin Mkapa kuongoza tume maalum ya kupambana na rushwa kama wewe wala sijawahi kuwa mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama wewe.
Sijui chochote kuhusu sheria, niponipo
tu naganga njaa mjini, nazugazuga ilimradi mkono uende kinywani na
maisha yasonge mbele. Hata hivyo, ningekuwa mimi kwenye nafasi yako,
kwa haya yanayoendelea kutokea hivi sasa, nakuapia kuwa kamwe
nisingevunjwa moyo wala kukatishwa tamaa na mamluki wa kisiasa
wanaokushambulia kila kukicha.
Ulipoteuliwa na Rais Kikwete kuongoza
tume ya mabadiliko ya katiba, kila mmoja alikutazama kama tumaini la
kweli la Tanzania ya kesho yenye ustawi katika kila sekta, kuanzia
sheria, utawala bora mpaka maendeleo ya mwananchi mmojammoja kupitia
katiba mpya ambayo wewe ndiye uliyepewa jukumu la kuzunguka kwa wananchi
na kuwasikiliza maoni yao juu ya katiba wanayoitaka.
Walioamini hivyo hawakukosea kwani uliifanya kazi yako ipasavyo na kudhihirisha kwamba ‘mtu mzima dawa’.
Walioamini hivyo hawakukosea kwani uliifanya kazi yako ipasavyo na kudhihirisha kwamba ‘mtu mzima dawa’.
Hata ulipokabidhi rasimu ya katiba hiyo
kwa Rais Kikwete na kuiwasilisha kwenye Bunge Maalum la Katiba kwa
mujibu wa kifungu 20 (3) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83,
kila mmoja alijua sasa mambo yatanyooka na Tanzania itajikwamua kutoka
hapa ilipokwama kwa zaidi ya miaka 50 tangu uhuru.
Maskini! Haikuwa hivyo, bunge lilipoanza
tu, kazi kubwa iliyotukuta uliyoifanya wewe na wajumbe wengine
waliokuwa kwenye kamati yako, ilianza kubezwa na kupuuzwa, kashfa na
maneno ya kuudhi yakaanza kutolewa, wakati mwingine yakikulenga moja kwa
moja.
Ukaitwa majina mengi mabaya kwa sababu
tu eti rasimu ya wananchi uliyoiandika ilionekana kuwa mwiba kwa vigogo
wenye uchu wa madaraka, wasiotimiza ahadi zao kwa wanacnhi na
wanaondekeza milungula na kujilimbikizia mali na kutupa maadili ya
uongozi.
Wengine wakawa wanakuvukia mipaka bila
kujali kwamba uelewa wako kwenye mambo ya sheria ni mkubwa na wa
kipekee, wakasau kwamba kiumri pia wewe ni baba au babu yao. Wengine
wakafikia mpaka hatua ya ‘kukuvuta sharubu’ hadharani.
Hata hivyo, mimi nikwambie kitu kimoja
mheshimiwa! Hizo kelele wanazokupigia zinamaanisha kwamba wewe ni mti
wenye matunda, lazima utapopolewa mawe tu mzee. Kamwe wasikukatishe
tamaa kwa sababu wewe ni shujaa wa kweli wa nchi hii usiyeogopa kusema
ukweli. Huku mtaani watu tunatamani hata ungekuwa bado kijana ugombee
wewe urais ili uiokomboe nchi hii. Wasalaam.
0 comments: