Zito atuhumiwa kuomba msaada wa kifedha kutoka iptl ili afifishe suala la escrow

Mwenyekiti wa PAC,Zitto Kabwe, atuhumiwa kuomba rushwa kutoka kwa mmiliki wa mtambo wa IPTL ili azime sakata hilo kupitia kamati yake.

Tuhuma hizo zimetolewa na katibu mkuu wa chama cha kijamii ambae amedai message ya Zitto kwenda kwa singasinga huyo ilinaswa.

Hata hivyo,mh.Zitto amekana tuhuma hizo na kudai kuwa maamuzi hafanyi peke yake na kwamba kashifa hiyo ni kubwa inayoweza kuangusha tembo mkubwa na hiki kinachoendelea hivi sasa kuhusu sakata hilo ni kishindo cha tembo huyo anaetaka kuanguka.

MY TAKE:
Pamoja na mapungufu ya Zitto, lakini kwa hili, sidhani kama ni kweli.

0 comments: