Kambi ya R-Kelly yamuita Alikiba ‘King of Tanzania’
Kambi ya muimbaji na mtunzi mahiri wa muziki wa R&B nchini Marekani, R.Kelly, imemuita Alikiba ‘King of Tanzania’.
Kambi hiyo inayojiita R.Kelly Media ambayo huendesha akaunti za mitandao ya kijamii yenye jina hilo, imepost picha ya Alikiba na R.Kelly kwenye Instagram zilizoandikiwa ‘King of Tanzania’ na ‘King of America’.
Hata hivyo, haijulikani kama akaunti hiyo iko chini ya R.Kelly mwenyewe au ni mashabiki wake tu wanaofanya promotion kwa mapenzi yao.
Mwaka 2010, R.Kelly aliandika na kutayarisha wimbo wa mradi wa Airtel One 8 na kushirikishwa wasanii mbalimbali wa Afrika wakiwemo Alikiba, Navio, 2Face Idibia, Fally Ipupa, Amani na wengine.
Wimbo uliitwa HANDS ACROSS THE WORLD.
0 comments: