Huyu ndie kijana wa CCM inayesemakana Kampiga Waziri Mkuu Mstafu Mzee Warioba na Chupa ya Maji Ubungo
Jambo la aibu na la kufedhehesha sana
limetokea leo katika mdahalo uliondaliwa na taasisi ya mwalimu
Nyerere,Ubungo. Katika mdahalo huo , vijana ambao mpaka sasa
hawajafahamika walisisima gafla wote kwa pamoja wakiwa na mabango
yanayopigia debe katiba inayopendekezwa na gafla fujo kubwa zikaibuka na
watu kuanza kupigana.
Kada wa CCM bwana Paul Makonda, pichani,
inasemekana alimpiga Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Mzee
Joseph Sinde Walioba kwa chupa ya maji. Hili ni jambo la kwanza la aibu
ya aina yake kutokea nchini kwa kijana mdogo kumpiga waziri mkuu wa
nchi na chupa ya maji. Tunatumai vyombo vya sheria vitachunguza tukio
hili na kuwachukulia hatu vijana wote waliohusika katika fedheha hii.
0 comments: